Matokeo ya mtihani yaliyotolewa hivi karibuni na taasisi ya Uingereza ya kuendeleza stadi za ujuzi wa ufundi ya City and Guilds, yameonyesha kuwa wengi wa washiriki wa mafunzo ya mradi wa kuimarisha ajira kupitia mafunzo ya ufundi nchini (EEVT), wamefaulu vizuri mtihani huo.Mtihani huo hutolewa na City and Guilds kwa vyuo mbalimbali duniani vinavyotoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi na wahitimu wake hupata vyeti vya kimataifa.Mradi wa EEVT nchini unaendeshwa kwenye Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta) vya Lindi na Mtwara, kwa ushirikiano wa Veta yenyewe, VSO na BG/LNG na unalenga kuboresha ajira za vijana kwenye mikoa hiyo na eneo lote la Kusini kwa ujumla.Aidha, mradi huo unalenga pia kukidhi ongezeko la mahitaji ya rasilimali watu wenye ujuzi kwenye sektaya gesi na huduma zinazohusiana na sekta hiyo, kulikosababishwa na shughuli za utafiti zinazoendeshwa na kampuni mbalimbali za gesi hasa katika maeneo hayo.Akizungumzia matokeo hayo, meneja wa mradi huo, Mawazo Mataje, alisema kati ya washiriki 76 waliofanya mtihani Januari 22 mwaka huu, Veta Mtwara washiriki 67 walifaulu sawa na asilimia 88.15.Alisema kati ya washiriki 54 waliofanya mitihani hiyoVeta Lindi, 46 sawa na asilimia 85.18 walifaulu.“Kuna uboreshaji mkubwa sana uliofanyika kutokanana ukweli kwamba, baadhi ya washiriki walifanya mitihani yote ya kuandika na ya njia ya mtandao inayohakikisha udhibiti wa ubora,” alisema.Mawazo alisema ujuzi unaofundishwa kwenye mradihuu ni pamoja na utayarishaji wa vyakula, ufundi mabomba, uchomeaji, ufundi seremala, ufundi magari na ufundi umeme.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni