Serikali yaondoa hoja Bungeni. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 31 Januari 2016

Serikali yaondoa hoja Bungeni.

Serikali imeamua kuondoa hoja yake Mapendekezo ya Mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka mitano bungeni, baada ya kujiridhisha kwamba kulikuwa na makosa wakati wa uwasilishwaji wake.Hoja hiyo iliondolewa jana jioni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kufuatia mabishano makali baina ya serikali na wabunge wa upinzani.Jana asubuhi Bunge lililazimika kukatisha kikao chake baada ya Kambi ya Upinzani kuibana serikali kwa kukiuka Katiba na kanuni za Bunge, kwa kuwasilisha kwenye chombo hicho Mapendekezo ya Mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka mitano badala ya Mpango wenyewe.Baada ya kikao hicho kuahirishwa, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe na yule wa Singida Mashariki, ambao ndio walioanza hoja hiyo Bungeni, walizungumza na waandishi wa habari na kumtaka Rais John Magufuli, kumwajibisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, kwa kuwa yeye ndiye mwenye wajibu wa kuishauri serikali.Kikao hicho kilianza tena jana jioni na ndipo Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliposema kuwa kabla ya kuruhusu hoja hiyo ya serikali kuwasilishwa, kwanza walitakiwa kukaa kama kamati ya mipango badala kuketi kama Bunge.Alisema pia Bunge lingepaswa kutengua kanuni kwa sababu Kanuni hizo zinaelekeza wakae Oktoba na Novemba kupitisha mpango huo.“Nilishtuka sana kwenye hoja ya kuvunja Katiba, baada ya haya niliyosoma ni wazi kuwa hakuna katiba iliyovunjwa kwa sababu wameleta hapa ili kuwashirikisha wananchi kupitia nyie," alisema Chenge."Baada ya kutafakari nimeona ni kweli Mpango haujaletwa, kwa hiyo naishauri serikali iondoe hoja iliyoileta kwa mujibu wa ibara ya 58 (5)."Kauli hiyo ya Chenge ilimwinua Dk. Mpango, ambayealiiondoa hoja aliyoiwasilisha kwenye meza ya Spikajana asubuhi.Baada ya kutoa hoja hiyo, Chenge aliahirisha Bunge mpaka Jumatatu.Kwa mujibu wa kanuni, Bunge lilijiwekea kufanya kazi mpaka siku ya Jumamosi lakini leo hakutakuwa na mkutano.Awali, Zitto na Lisu walisema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mpango, anatakiwa kuwajibishwa kwa sababu licha ya kufanya kazi Tume ya Mipango kwa miaka mitano, ametela bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Miaka mitano ili ujadiliwe ili hali Katiba na Kanuni zinataka chombo hicho cha kutunga sheria kijadili Mpango wa Maendekeo na siyo mapendekezo.Baada ya Mwenyekiti Chenge kusikiliza miongozo hiyo alimkaribisha mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia, ambaye baada ya kusoma hotuba yake alimkaribisha tena Msemaji wa Upinzani kwenye Wizara ya Fedha, Mbunge wa Mwomba David Silinde.Silinde alisema kwa kuwa serikali imekiuka Katiba Ibara ya 63 (3) (C), na Kanuni ya Bunge 94 (1) kambiya upinzani haitowasilisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa kwa miaka mitano, mpaka serikali itakapowasilisha wa kwake kama ambavyo Katiba na kanuni zinataka.Kutokana na hali hiyo, Chenge alilazimika kuahirishaBunge saa 6:25 mchana badala ya saa 7:00 kama ambavyo kanuni zinaelekeza.Vurumai iliponziaAkiomba mwongozo kwa meza ya Spika, Zitto alisema waziri wa fedha ametoa hotuba ya Mapendekezo ya Mwelekeo wa Maendeleo wa miakamitano 2016/17 mpaka 2020/21 na hajatoa hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendelo wa Mwaka 2016/17.“Maelezo ambayo umeyatoa ili kutuongoza kwenye kuchangia ambayo umeyatoa kanuni ya 94 (1) (4), ni maelezo ya mwaka mmoja, hayahusiani na mpango wa miaka mitano, tunajadili mpango huu kwa masharti ya katiba, Ibara ya 63 (3) (C),” alisema Zitto."Bunge hujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu, au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamuhuri ya Muungano na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpangohuo."Zitto alisema mwenyekiti wa Bunge ametoa maelekezo ya kuchangia hotuba hiyo akitumia Kanuni 94 ya Bunge ambayo inazungumzia Mpango wa mwaka mmoja mmoja.“Kanuni zinakukataza kuwahisha shughuli za bunge, hapa hatujadili mpango wa mwaka mmoja, tunachokijadili kwa sasa ni mpango wa miaka  mitano ambao itabidi tuutungie sheria, alafu ndiyo tuje kwenye huo utaratibu ambao upo wewe unaueleza."Maelekezo yako yanakiuka kanuni, hayajafuata uataratibu na hapa waziri hajatuletea mpango, ameleta mwelekeo wa mpango, Bunge halitakiwi kujadili mwelekeo wa mpango, na wabunge naomba tuelewane katika hili."Hili ni suala la nchi yetu siyo suala la chama,  serikali mkiruhusu mjadili mwelekeo wa mpango mnajidhalilisha, mnapaswa mjadili mpango wa maendeleo wa miaka mitano, na mpango huu unapaswa kutungiwa sheria,” alisema.Alisema moja ya matatizo ya kutotekelezwa mpango uliopita ni kwa sababu Bunge halikuutungia sheria kama ambavyo inatakiwa na Katiba.Baada ya maelezo hayo, Chenge alisimama na kusema amesikia na anahitaji muda ili aweze kutoa ufafanuzi.Chenge baada ya kutoa maelezo hayo, alimruhusu Lisssu kuomba mwongozo wake.Lissu alianza kwa kusoma orodha ya shughuli za Bunge kwa jana ambapo kwenye ukurasa wa 11 ilikuwa ikisema ‘Bunge litajadili na kuidhinisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha mitano 2016/17- 2020/21’.Baada ya kusoma eneo hilo alisema, “Mpango wa pili wa Maendeleo kwa kipindi hicho uko wapi? Haujawasilishwa."Kanuni ya 94 (1) ya Kanuni za kudumu za Bunge lako tukufu, inasema ‘Bunge litakaa kama kamati ya mipango ili kukidhi matakwa ya kanuni ya 63 (3) (c) ya Katiba’.“Tutakaa kwa siku tano hapa tutajadili na kuidhinisha mpango na kuitungia sheria, mswada washeria husika uko wapi? Tutaupitisha lini? Mswada hauopo, mpango haupo, tunajadili kitu gani?”Alisema pia Chenge amewaeleza wabunge kwamba baada ya mjadala kamati ya bajeti ndiyo itakayopelekewa mpango.“Nilikuwa naangalia shughuli za kamati ya bajeti, aya ya tisa na nyingine, labda nina matatizo ya macho lakini ukurasa wa 38 ambapo kazi za kamati ya bajeti zimetajwa, sijaona mahali ambapo kamati hii ina mamlaka au majukumu ya kupokea na kujadiliwa mpango wa maendeleo wa taifa."Hili Bunge lako tukufu linahitaji kuongoza sawasa, nina wasiwasi kama unaliekeleza Bunge sawasawa,”alisema Lissu.Chenge alimkatisha Lissu na kusema hoja yake na ile ya Zitto zinafanana na tayari maelezo yake alishayatoa.Nje ya BungeNje ya ukumbi wa Bunge, Zitto na Lissu walizungumza na waandishi wa habari ambapo Lissu alisema serikali ilianza kuvunja kanuni kwa kutotoa mpango huo siku saba kabla ya mjadala kama ambavyo kanuni zinataka.Alisema kazi ya kwanza ya serikali baada ya kutoka kwenye uchaguzi ni kuwasilisha Mpango wa Taifa wa kila mwaka na wa miaka mitano.Alisema jambo hilo lipo kikanuni na linalindwa na Ibara ya 63 (3) ya Katiba hivyo kazi ya Bunge ni kujadili Mpango huo na kuuidhinisha.“Sasa wanataka kufunika kombe kama alivyokuwa anataka mwenyekiti, miaka mitano iliyopita kwa sababu ya udhaifu wa serikali hatukutunga sheria ya kutekeleza mpango uliopita.“Ukosefu wa weledi wa serikali ya iliyopita umehamia kwenye hii ya hapa kazi tu, leo Bunge kwamujibu wa orodha ya shughuli za leo (jana) wanasema Bunge lijadili Mpango na siyo mwelekeo wala mpango wa muda mfupi,” alisema Lissu.Alisema yote hayo ni matokeo kamati kuvurugwa, hililisingetokea kama wabunge wa kamati za bajeti waliopita wangekuwepo.“Tusingie kwenye hii aibu kwa sababu kwa sasa hakuna mpango, hakuna sheria, siku tano hizi tutajadili kitu gani? Tutatunga sheria ya kitu gani? Hapa ni kuvuruga ili serili ya hapa kazi tu isihojiwe,” alisema Lissu.AG ni JipuAlisema kutokana na Ibabara ya 59 (3), Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mwenye jukumu la kuishauri serikali ili itemize vyema majukumu yake.“Mwanasheria mkuu wa Serikali ndiye anayeandaa mswada wa serikali, ndiye mwenye kuishauri juu ya masuala muhimu kama haya."Tangu mwaka jana tumesema, Gorge Masaju hawezi kuvaa viatu vya mwanasheria mkuu, hana uwezo na uthibitisho kwamba hivyo viatu ni vikubwa mno kwa mtu kama yeye ni huu."Kama kuna jipu kubwa kwenye baraza ni mwanasheria mkuu, hana uwezo wa kutimiza majukumu yake, ushauri wa bure Magufuli amtafutie AG kazi nyingine ya kufanya siyo hii, hivyo viatu kwake ni vikubwa mno, wa pili ni Waziri wa fedha."Lissu alisema tangu Bunge kuanza maamuzi yamekuwa yakifanywa na Ikulu na kwamba hata kamati za Bunge zinadaiwa kungenezwa na muhimilihuo mwingine.“Wabunge wa CCM wametishwa, wenye uelewa wamepelekwa kwenye kamati za ukimwi, sheria ndogo maendeleo ya jamii, kazi ya kwanza wameshindwa inabidi waondoe hii kitu,” alisema Lissu.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa