Majaliwa akuta ufisadi bn 21/- bandari Tanga - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 21 Februari 2016

Majaliwa akuta ufisadi bn 21/- bandari Tanga

Baada ya kukaribia kusafisha ya Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, jana aliibuka ghafla katika Bandari ya Tanga na kukuta ufisadi unaozidi Sh. bilioni 21.5Kutokana na uozo huo, Majaliwa alimpa masaa 18 Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mkoa wa Tanga, Henry Arika kuwasilisha barua yenye maelezo na sababu kamili za kuagiza tishari tatu ambazo ni mbovu.Tishari ni vyombo vinavyotumika kupakulia mizigo kwenye meli kubwa zinazoshindwa kufika kwenye bandari zenye kina kidogo cha maji kama Tanga.Matishari hayo yaliyonunuliwa na Mamlaka hiyo kwaDola za Marekani milioni 10 (sawa na zaidi ya Sh. bilioni 21.5) hayafanyi kazi kwa miaka minne sasa.Waziri Mkuu alimtaka Meneja huyo akubali makosa yaliyojitokeza wakati wa manunuzi ya matishari hayo, au ajiondoe kazini mwenyewe kabla hatua mbalimbali hazijachukuliwa dhidi yake.Majaliwa alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake ya ghafla kwenye Bandari hiyo muda mfupi tu baada ya kutoka katika mazishi ya baba wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Ummy Mwalimu, yaliyofanyika katika kijiji cha Mchukuuni, Jijini Tanga.“Meneja nataka mpaka kesho (leo) saa sita nipate maelezo yako kama unahusika au huhusiki, na kamawewe binafsi hauhusiki uniambie nani hasa alihusikakuagiza matishari haya feki ambayo yameendelea kuwa mzigo mkubwa na kuzorotesha utendaji wa Bandari ya Tanga,” alisema.Alisema kutokana na ufisadi huo, serikali imeendeleakutumia fedha nyingi katika gharama za mafuta ya petroli yanayotumika kutokana na vyombo vya kukokota matishari hayo.Waziri Mkuu alihoji kwanini Mamlaka hiyo Mkoa wa Tanga iliwasilisha maombi ya matishari mawili na badala yake TPA ikapeleka matatu, ambayo tangu yalipowasili bandarini hapo kwa zaidi ya miaka minne sasa hayaweza kufanya kazi kutokana na ubovu.“Ninyi mmeomba mawili wao wakawaletea matatu ambayo ni madogo na yametumika, siyo mapya na hayajiendeshi mpaka yasukumwe,” alisema.Aidha, Waziri Mkuu aliitaka Menejimenti ya TPA kuhakikisha inaanzisha karakana kwa ajili ya matengenezo ya vifaa mbalimbali na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani hasa vijana wanaotoka vyuoni kwa lengo la kuepuka kufanya matengenezo Mombasa nchini Kenya na kuongeza gharama kwa serikali zisizo za lazima.Katika maelezo yake, Meneja wa TPA Mkoa wa Tanga, Arika alisema yeye ni mgeni na wakati vifaa hivyo vikiagizwa hakuwepo na kamwe hakuhusika kwenye mchakato wa manunuzi ya matishari hayo.Kwa upande wake, Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Tanga, Felix Mtui, alisema walipeleka mahitaji yao TPA Makao Makuu ambao ndiyo wenye jukumu la kusimamia mchakato wote wa manunuzi.Wakati huo huo, Waziri Mkuu aliagiza Mamlaka ya Bandari kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Tanga (TRA) na Jeshi la Polisi kudhibiti sukari inayoingia hapa nchini kupitia njia za panyakwenye Bandari ya Tanga kinyume cha utaratibu hatua ambayo inakosesha serikali mapato na kutishia usalama wa afya za walaji.“Mkuu wa Mkoa hapa Tanga kupitia Bandari ya Tanga na bandari bubu zilizopo kunaingia sukari nyingi sana kutoka nje ya nchi sukari ambayo haijapiwa na TBS, TFDA,” alisema Majaliwa.“Na hakuna anayejua inaathari kiasi gani kwamatumizi ya binadamu hivyo naagiza TRA, TPA na Polisi kuhakikisha mnaimarisha doria na tutaleta magari mapya kwa ajili ya hilo ili jambo hili lifikie ukomo.”Alisema kwa mtu yeyote atakayekamatwa kuhusika na uingizaji wa sukari hapa nchini kutoka nje ya nchi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.Kwa mujibu wa Kiongozi huyo ni kwamba viwanda vine vya sukari vinazalisha zaidi ya tani 420,000 kwamwaka ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya nchi nzima.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa