Yanga itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya pili ya watani wa jadi msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Oktoba mwaka jana kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, ukiwa ni ushindi wa kwanza dhidi ya timu hiyo ya Msimbazi tangu Mei 18, 2013 walipata matokeo kama hayo.Matokeo mabaya katika mechi zinazokutanisha timu hizo kongwe zaidi katika ligi ya Bara mara nyingi yamekuwa yakigeuka shubiri kwa makocha, wachezaji na hata viongozi wa klabu hizo.Uongozi wa juu wa Yanga, kwa mfano, ulilazimika kuachia ngazi baada ya kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya watani wao jadi Mei 6, 2012. Pia uongozi wa timu hiyo ya Jangwani ulimtimua aliyekuwa kocha mkuu Mdachi Ernie Brandts na watendaji wengine wote wa benchi la ufundi baada ya kufungwa 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya ‘ndondo’ ya ‘Nani Mtani Jembe’.Kipigo hicho hakikuishia kwa benchi la ufundi, baadhi ya wachezaji akiwamo kipa Juma Kaseja walipata wakati mgumu wa kuzushiwa kucheza chiniya kiwango huku mlinda mlango huyo wa sasa wa Mbeya City FC akidaiwa pia kuruhusu bao la kizembe.Mechi ya leo kati ya timu hizo inatarajiwa kutoa picha ya timu itakayotwaa ubingwa wa ligi ya Bara msimu huu. Simba ndiyo inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na mtaji wa pointi 45 baada ya mechi 19 ikifuatwa na Yanga ambao wana pointi 43 baada ya mechi 18.Nipashe tunatambua kuwapo kwa presha kubwa kutoka kwa mashabiki, wanachama na hata viongoziwa timu hizo, lakini ni vema kuwakumbusha kuwa ‘mtu wa mpira wa miguu ni lazima akubaliane na matokeo yake ya kushinda, kushindwa ama sare, vinginevyo hana sababu ya kujihusisha na soka’.Hatutarajii kuona kocha au kiongozi anatimuliwa au kuangushiwa ‘jumba bovu’ kutokana na matokeo ya mabaya ya mechi ya leo, kama ilivyofanyika katika miaka kadhaa iliyopita.Nipashe hatutarajii kuona tena Yanga ama hata watani wao Simba wakitoa ‘kafara’ kwa kuwabebesha mzigo ama kuwatimua wachezaji kutokana na matokeo ya leo badala yake matarajio yetu ni uongozi kuelekeza makocha kutumia mchezo huo kuimarisha safu ambazo zitaonekana kuwa na udhaifu.Tunatambua Simba iliyoshinda mechi zote saba za Ligi Kuu ilizocheza mwaka huu, itashuka kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa na presha kubwa ya kutaka kulipa kisasi cha kufungwa duru la kwanza msimu huu, wakati Yanga ikitaka kuendeleza rekodi yao ya ushindi, lakini ahueni ya mechi hiyo ni sare.Hilo linatokana na viongozi wa timu hizo mara nyingihukosa msimamo na kuziongoza kwa kutazama wapi upepo unapoelekea, hivyo kulazimika kutoa ‘kafara’ kwa kubebesha wachache ama makocha zigo la matokeo ili kupata pakupumulia. Lakini tunatoa rai kwa viongozi wa klabu hizo kukumbuka kwamba kuna zaidi ya mechi 10 zitakazokuwa mbeleyao kabla ya kumalizika kwa msimu huu, hivyo ‘vurugu’ na timuatimua ya aina yoyote itawazigharimu timu zao katika mbio za ubingwa wa ligi ya Bara.Ni matarajio yetu kuona sasa viongozi wa Simba, Yanga wakiegemea katika kuamini kushinda, kushindwa ama sare kama ilivyo matokeo ya mchezo wa soka.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni