Tukio Kubwa Nyumbani Kwa Lowassa - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatano, 30 Machi 2016

Tukio Kubwa Nyumbani Kwa Lowassa

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia naMaendeleo (Chadema),Freeman Mbowe, amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa; na kwamba matokeo hayo yawe chachu ya kufanya  vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.Amesema uchaguzi si tukio, bali mchakato; na kwamba kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasaya urais,  watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi na matokeo yake. Alisema matokeo hayo yanapswa kuwatia hasira na kuwahamasisha waendelee kupambana,Mbowe aliyasema hayo Masaki, nyumbanikwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajiliyake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,”amesema Mbowe.Aliongeza kwamba, kazi ya mapambano wanayofanya viongozi sasa ina manufaa kwa kizazi kijacho, na kama wanaoifanya sasa wakafanikiwa kuonja matunda ya kazi ya mikono yao basi ni jambo la kumshukuru Mungu.“Kazi anayofanya Lowassa (Baba Kadeti) si lazima aone matunda yake leo, huenda mtoto wake ataonja na asipoonja Kadeti basi wajukuu wataonja matunda hayo na kutambua mchango mzuri wa babu yao kwa kazi kubwa ya maana anayofanya sasa,”amesema.Aliwahimiza Watanzania zaidi ya 600 waliokuwepo kwenye halfa hiyo kuwa walewalio wafuasi wa vyama vya siasa hata wasio na vyama wana wajibu wa kuendelea kwa nguvu zote na kazi ya kupambana ambayo Lowassa amejiunga nayo, kwani wakati wa uchaguzi watu wengi walipigana kumsaidia sio kwa ajili ya familia yake ila walifanya vile kwa sababu ya nchi hii, huku Lowassa akiwa kiongozi na mpeperusha bendera.Mbowe alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania waendelee kumwombea neema, ujasiri na afya njema Lowassa kwani taifa bado linamhitaji kuliko pengineanavyohitajika na familia yake.Aidha, Mbowe alimsifu pia Regina, mke waLowassa, kwa ujasiri wake na familia nzima kwa uamuzi mzuri na ujasiri aliochukua katika kuhakikisha Watanzaniawanatafuta haki na ujasiri kwa kukata minyororo ya watesi.“Mama ulikuwa mwoga kwenye kampeni katika hatua za awali, lakini baadaye ulipata ujasiri kama mgombea mwenyewe.Asante sana kwa kuondoa woga; asante kwa kuongoza familia, na sasa tuendelee na mapambano.”alihimiza MboweKabla ya Mbowe kusimama, neno la kuwashukuru watu waliofika nyumbani lilitolewa na Regina akasema familia, hasaLowassa mwenyewe, ilikuwa inasubiri kwahamu siku ya kumshukuru Mungu na Watanzania kwa mazuri mengi aliyowatendea.Hafla hiyo ya shukrani ilianzia kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Dar es Salaam. Lilichagizwa na nyimbo kadhaa za shukrani zilizopendekezwa na Lowassamwenyewe, na kuimbwa na washiriki wote, wakiwamo wa madhehebu mengine ya dini.Miongoni mwa washiriki wa hafla hiyo ni baadhi ya wanachama wapya wa  UKAWA waliojiengua CCM mwaka jana, wakiwamo Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Lawrence Masha, John Guninita, na wengine.Ilihudhuriwa pia na wanasiasa, viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, vijana na wazee, matajiri na watu wa kawaida kutoka sehemu mbalimbali.“Tumepata mengi mazuri, tunaweza kusafiri kwenda Monduli na kurudi si sababu tuna magari mazuri kuliko wengine; tunaweza kusafiri kwa ndege na tukarudi salama, lakini hata wakati mwingine unasikia mtu anakupigia simu kukusalimu au kukuandikia ujumbe mzuri wa faraja, haya yote  ni sababu ya Mungu na tukaona leo tufike Kanisani kusema Mungu asante kwa mema yote uliyotujalia,”alisema Regina akiwa amejawa tabasamu muda wote, huku akishangiliwa.Wajukuu wa Lowassa walijumuika kumwimbia babu yao wimbo kutoka miongoni mwa tenzi za Injili zilizoandaliwakwa ajili hiyo, huku wakiongozwa na mpiga kinanda.Baada ya wajukuu, Masha alitumbuiza washiriki kwa wimbo wa Kiingereza “Amazing Grace,” akatuzwa kiasi cha Tsh. 50,000 ambacho, hata hivyo, alikigawa kwa wajukuu wa Lowassa.



Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa