Wananchi wametakiwa kutoa taarifa dhidi ya askari ambao wanadaiwa kuwafumbia macho wanaojihusisha na biashara za dawa ya kulevya ili wachukuliwe hatua.Wito huo ulitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dk. Abdallah Possi, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum,Mwantumu Haji, aliyehoji ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya askari ambao wanafumbia macho wauza dawa za kulevya.Haji alisema kuna askari ambao hawaendani na kasiya kuthibiti dawa za kulevya na kuhoji ni mbinu gani zinazotumika kuthibiti tatizo hilo.Dk. Possi alisema askari kutochukua hatua shidi ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na kufanya hivyo ni kosa la jinai.“Kwa wale ambao wanawafahamu askari wanaojihusisha na suala hili watoe taarifa ili wachukuliwe hatua,” alisema.Aidha, akijibu swali la msingi la mbunge huyo, aliyehoji serikali imejipanga vipi kunusuru vijana katika janga la utumiaji wa dawa za kulevya, Dk. Posi alisema serikali inatambua maumizi ya dawa zakulevya yana madhara mengi kwa watumiaji, familia na jamii kwa jumla, hivyo imejipanga kupambana na tatizo hilo.Alisema ili kuwanusuru vijana serikali imechukua hatua kwa kuongeza juhudi za kimkakati za kuhakikisha wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanakamatwa na kuadhibiwa vikali.Alisema serikali pia inaendelea kutoa matibabu kwa watumiaji wa dawa za kulevya katika hospitali na vituo vya magonjwa ya akili nchini ili kuwasaidia watumiaji wa dawa hizo kuacha.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni