Waziri wa Mkapa ataka Z'bar iachwe ijiamulie mambo yake. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatano, 3 Februari 2016

Waziri wa Mkapa ataka Z'bar iachwe ijiamulie mambo yake.

Mwanasiasa mkongwe Zanzibar, Ali Ameir Mohamed, amesema Zanzibar ni nchi huru inayojitegenea ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo  haipaswi kuingiliwa wala kuhojiwa katika mambo yake ya ndani, ikiwamo suala la kurudiwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakaofanyikaMachi 20, mwaka huu.Akizungumza na Nipashe mjini hapa jana, Ali Ameir alisema Zanzibar ina madaraka yake, katiba  yake, Rais wake, Baraza la Wawakikishi na mahakama, hivyo haipaswi kuingiliwa katika mambo yake licha ya kuwa shemu ya Tanzania.Alitoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa  tamko la nchi saba za Jumuiya ya Ulaya zikiongozwa Marekani, kuwa hawajaridhishwa na kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.Alisema mabalozi wanaowakilisha mataifa yao nchini lazima wafahamu na kutambua kuwa Zanzibar ni nchi huru na ilipata uhuru wake uliootokana na Mapinduzi yaliouangusha ufalme wa kigeni uliokalia  visiwa hivyo kwa miaka 160.Alisema kitendo cha mabalozi wa nchi nyingine kuhoji uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza kurudia uchaguzi ni kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar, kwenda kinyume cha  taratibu za kidiplomasia na ukiukaji wa mikataba ya kimataifa.Alisema katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeipa mamlaka ZEC kuratibu, kuitisha, kusimamia na kutangaza matokeo ya uchaguzi na kwamba maamuzi yake  hayawezi kuhojiwa au kuingiliwa na mtu au mamlaka yoyote iwe ya ndani au nje ya nchi.Alisema uamuzi uliofanywa za ZEC kuitisha uchaguzi wa marudio unapaswa kuheshimiwa kwa sababu yanatokana na utashi wa katiba na sheria nakwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kukwamua utata wa mkwamo wa uchaguz mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa