Serikali ichukue hatua kuwakinga Watanzania na ugonjwa wa zika. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatano, 3 Februari 2016

Serikali ichukue hatua kuwakinga Watanzania na ugonjwa wa zika.

Serikali imetoa taarifa ikiwatoa hofu Watanzania juu ya kuzuka kwa ugonjwa hatari wa zika nchini.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu, alikaririwa na gazeti hili jana akisema hakukuwa na taarifa ya Mtanzania yeyote kushikwa na ugonjwa huo.Ummy alitahadharisha Watanzania kuhakikisha wanapima afya pale watakapojisikia homa ili kufahamu kama wana vimelea vya ugonjwa huo.Ugonjwa huu ambao umesambaa kwa sasa katika nchi za Amerika Kaskazini, Kati na Kusini, uligundulika mwishoni mwa mwaka jana nchini Brazil kisha na kusambaa kwa kasi katika nchi zingine za Amerika Kusini, Amerika ya Kati na visiwavya Caribbean.Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa kuna hatari ya ugonjwa huo kusambaa na kuwapata watu wengi zaidi.Hali hiyo inachochewa zaidi kutokana na kusambaa kwa mbu wanaoeneza ugonjwa huo, ambao wanajulikana kwa jina la Aedes Aegypti. Mbu hawa wamezaliana kwa winga kwenye nchi za Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean.Kuna wagonjwa pia waliopatikana nchini Marekani na kuongeza wasiwasi zaidi wa kusambaa ugonjwa huu katika sehemu mbalimbali duniani.Hata hivyo, serikali inasema imechukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.Dalili zinazojulikana zaidi za ugonjwa ni zile za kuumwa homa na kuwashwa.Aidha, ugonjwa huo una hatari zaidi kwa wajawazito kwa kuleta madhara kwa watoto wanaozaliwa kutokana na wanawake walioambukizwa na ugonjwa huo.Serikali inasema dalili za ugonjwa huo zinafanana nazile za ugonjwa wa dengue. Dalili hizo ni pamoja na homa kali, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo, macho kuwa mekundu na vipele vidogo vidogo kamaharara.Viashiria hivyo huanza kujitokeza katika siku mbili hadi saba tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya zika.Njia ya kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na kutumia dawa ya kupaka ili kuzuia mbu na kuvaa nguo zinazofunika mwili mzima. Pia ni muhimu kwa watu kuhakikisha hawatoi nafasi kwa mbu wanaoeneza ugonjwa wa zika kuzaliana.Mbu hawa mara nyingi huzaliana kwenye ndoo zenye maji, maua na matairi.Kutokana na kuwepo kwa tishio hilo, tunashauri serikali ichukue hatua za dhati ili kuepusha taifa kukumbwa na ugonjwa huu.Suala la usafi wa mazingira na kuzuia maji kutuama ni muhimu katika kuzuia kuzuka kwa  ugonjwa huu, jambo ambalo linatakiwa kusimamiwa na taasisi za serikali.Ni jambo muhimu kwa wananchi kupatiwa huduma muhimu za kijamii katika sehemu safi na kutokuwepo kwa maeneo yanayosababisha maji kusimama.Nchi zilizoendelea zimefanikiwa kuzuia kuzuka kwa magonjwa kama zika kutokana na kuhakikisha zinaweka kipaumbele suala la usafi wa mazingira.Katika miaka ya mwanzoni mwa uhuru, serikali iliweka kampeni kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ya maji safi na kulikuwa na ujenzi wa mabomba katika sehemu mbalimbali nchini.Matokeo yake miundombinu ya maji safi ni ile iliyoachwa na mkoloni na juhudi si kubwa za kupanua wigo wa utoaji maji safi.Pia nchi yetu imekuwa inakabiliwa na matatizo ya kuzuka kwa magonjwa yanayotokana na uchafu kama kipindupindu kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya majitaka.Katika miji mingi ya Tanzania kuna tatizo kubwa la uchakavu na ukosefu wa miundombinu ya majitaka. Kutokana na hali hiyo, serikali inapaswa  kuongeza jitihada za kuhakikisha suala la usafi linapewa uzito.Sasa tunahimiza kuwepo kwa jitihada za makusudi za serikali na vyombo vyake kuhakikisha vinakuwa na kampeni kamambe ya kuzuia ya kuingia nchini kwa ugonjwa wa zika.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa