Kampuni ya TBL Group imewatunukia vyeti na zawadi wafanyakazi wake ambao wameitumikia kwamuda mrefu.Wafanyakazi hao wanaofanya kazi katika viwanda vyake vya Konyagi, Chibuku na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) walitunukiwa zawadi hizo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, jijini Dar es Salaam.Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Ufundi. Gavin Van Wijk, aliwapongeza wafanyakazi kwa uvumilivu na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utumishi wao.Wijk alisema kampuni hiyo itaendelea kuwajali wafanyakazi wake na kuwajengea mazingira bora yakazi kwa lengo la kutoa mchango mkubwa zaidi kwa taifa kwa taasisi na taifa kwa ujumla."Tunaamini kuwa wafanyakazi wetu wote ni familia moja hivyo siku zote tutakuwa nao karibu na kuendelea kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi. Naamini sote tukishirikiana tutafanikiwa na kuendelea kupata mafanikio," alisema.Kwa upande wake, Meneja wa TBL kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alisema wafanyakazi hao ni mfano wa kuigwa na kuwataka wengine, hususani vijana, kufanya kazi kwa bidii na kuwa wavumilivu."Tuko hapa kwa ajili ya kuwapongeza wenzetu ambao wamefikia siku hii kupewa tuzo ya utumishi wa muda mrefu. Ninaamini sote tukifanya kazi kwa bidii na kuwa na uvumilivu, tutafanikiwa kufikia hatua kama waliyofikia wenzetu ambao tunawapongeza,” alisema.Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake waliotunukiwa vyeti, Sylvester Kunambi ambaye ametumikia kampuni kwa miaka 35, alisema siri kubwa ya utumishi wa muda kwenye kampuni ya TBL ni kutokana na mazingira bora ya kazi .Wafanyakazi 25 waliotumikia kampuni katika kipindi cha miaka 10 mpaka miaka 35 walitunukiwa vyeti.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni