Serikali yatakiwa kupunguzia wafanyakazi mzigo wa kodi. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 28 Januari 2016

Serikali yatakiwa kupunguzia wafanyakazi mzigo wa kodi.

Serikali  imetakiwa kupunguza makato ya kodi kwa wafanyakazi wanaokatwa makato ya juu yanayofikiaasilimia 30.Rai hiyo ilitolewa bungeni mjini hapa jana na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Chakoma, wakati akiuliza swali la nyongeza, akitaka kujua kama serikali ina mpango wowote kwa wafanyakazi ambao wana makato makubwa ya kodi yanayo fikia asilimia 30.Akijibu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti yaUtumishi wa Umma na Utawala Bora), Angelah Kairuki, alisema wizara yake imeshawalisha mapendekezo ya kupunguza kodi kwenye kamati ya kikosi kazi (Taxsiforce) kwa ajili ya kulijadili suala hilo.Alisema kikosi kazi hicho hicho kinajumuisha Wizaraya Fedha na Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutekeleza jambo hilo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.Akijibu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, AshantuKijaji, alisema, mfumo wa kodi ya wafanyakazi uliopo sasa umeweka viwango kwa kuzingatia kipatocha mfanyakazi ambapo kiwango cha kodi hupanda kadri ya kipato cha mfanyakazi kinavyopanda.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa