Mvutano wa suala la hoja iliyowasilishwa kuhusu Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ulisababisha vurugu kiasi cha uongozi wa bunge kuamuru walinzi wa bunge, polisi na mbwa kutumika kudhibiti hali kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma.Jambo la kusikitisha zaidi ni kitendo cha mbwa kupelekwa nje ya jengo la bunge kwa ajili ya kutumika kuwatoa wabunge wa upinzani.Matumizi ya polisi na mbwa katika kudhibiti baadhi ya wabunge kumeleta picha mbaya mbele ya wale wote wanaoamini katika demokrasia.Wabunge wa vyama vya upinzani walikuwa wanapinga hatua ya uongozi wa Bunge kukataa hojaya kusitisha shughuli zingine za bunge ili kujadili suala la TBC kusitisha matangazo ya moja kwa mojaya vikao vyao.Hali katika ukumbi wa bunge haikuwa shwari kwani walinzi na polisi walijazana mithili ya kuwa walikuwawanakabiliana na wahalifu sugu. Kitendo cha polisi hao kujazana ndani ya ukumbi wa bunge kilikuwa uvunjaji wa wazi wa kanuni za bunge.Ni mara ngapi tumesikia wabunge wakiombwa kanuni zitenguliwe ili viongozi wa kitaifa waruhusiwekuingia ndani ya ukumbi wa bunge? Ilitokea hata mwaka jana wakati Rais Dk. John Magufuli alipohutubia bunge kwa mara ya kwanza wakati viongozi mbalimbali walipoombewa kuingia ndani yaukumbi wa bunge.Taifa zima juzi lilishuhudia askari wakijazana ndani ya ukumbi wa bunge, tena bila utaratibu maalum kwa ajili ya kukamata wabunge.Mara nyingi tumetahadharisha kabla ya bunge hili kuanza kuwa kunahitajika busara ya kiwango cha juu kutoka katika kiti cha spika katika uendeshaji wa bunge.Kitendo cha kukosekana kwa maridhianio kati ya kiti cha spika na baadhi ya wabunge kumefanya bunge hili kugeuka kuwa uwanja wa malumbano. Tangu kuanza kwa bunge hili, Jumanne iliyopita, kumekuwana malumbano kila kukicha na kusababisha vurugu.Mathalani, kuna kamati za bunge hazina wenyeviti kutokana vyama vya upinzani kususa kwa kupinga utaratibu wa uteuzi wa kamati zenyewe. Pia vyama vya upinzani havijateua mawaziri kivuli kutokana na tofauti baina yao na spika.Taifa letu linakabiliwa na changamoto nyingi ili kupiga hatua kimaendeleo na bunge ni taasisi muhimu katika kuisimamia serikali. Hata hivyo, tunachokiona hapa kuna mvutano mkubwa baina ya pande mbili ambazo zinakinzana kimsimamo.Kuna kundi la kwanza ambalo linaweka mazingira yakudhibiti nguvu ya bunge kufanya kazi zake na kundi la pili linalotaka bunge liwe chombo cha kuibana serikali.Watu wengi walikuwa wanategemea kuona bunge hili likianza kwa kishindo katika kazi zake za kuisimamia serikali lakini hali imekuwa tofauti.Serikali ya awamu ya tano ilianza kwa nguvu katika utekelezaji wa kaulimbiu yake ya `Hapa Kazi Tu’ na tumeshuhudia hatua mbalimbali zikichukuliwa ili kuimarisha utendaji wa serikali.Bila shaka bunge lingekuwa msaada mkubwa katika kuiunga mkono serikali kwa kuanika udhaifu wa serikali.Kumekuwa na malalamiko mengi tangu kuanza shughuli za bunge mwaka jana, mathalani kuanzia uchaguzi wa Naibu Spika hadi kwenye kuunda kamati.Hatua hizi zimeanza kujenga dhana potofu kuwa pengine kuna baadhi ya wakubwa wanataka kukata makali ya bunge katika kuibana serikali.Hali hii inaleta hofu ya kurudisha lile bunge la enzi yamfumo wa chama kimoja ambalo lilikuwa likifanya kazi kama muhuri wa serikali badala ya kuisimamia.Wabunge wa vyama vya upinzani kwa sasa wamegoma kuchangia mjadala wa hotuba ya Rais, ambayo ilikuwa muhimu katika kujenga msingi wa utendaji wa serikali ya awamu ya tano.Ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawia na majukumu ya mhimili huo kutekelezwa, uongozi wa bunge badala ya kuendekeza kutumia nguvu tu, unatakiwa kutafuta maridhiano na wabunge wote ili bunge lifanye kazi zake inavyopasa.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni