Mbunge ashangazwa na huduma mbovu hospitali ya wilaya Pangani. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 28 Januari 2016

Mbunge ashangazwa na huduma mbovu hospitali ya wilaya Pangani.

Mbunge wa Pangani (CCM), Jumaa  Aweso, amefanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani na kukutana na upungufu kadhaa.Ziara ya mbunge huyo hospitalini hapo, ilikuwa na lengo la kukagua uwajibikaji wa watumishi pamoja na changamoto wanazokutana nazo.Aweso  baada kutembelea kila kitengo hospitalini hapo,  alieleza kutoridhishwa na huduma zinazotolewa  katika  na kwamba zina upungufu mwingi ikilinganishwa na mategemeo ya wananchi kwa kuwa ndiyo hospitali kubwa wilayani hapo.Alitaja baadhi ya upungufu aliokutana nao ni pamoja na kutofanya kazi kwa mashine ya x-ray na baadhi ya mashine za maabara, jengo la upasuaji kuvuja na uhaba wa vifaa tiba.Kutokana na hali hiyo, alisema atawasilisha kunakuhusika ili serikali  ichukue hatua za haraka kunusuru maisha ya wananchi wa wilaya hiyo.Aweso alieleza kushangazwa na uchakavu wa jengo la upasuaji hadi kufikia hatua ya  kuvuja pamoja na kukosekana kwa vifaa hivyo muhimu  na kudai kuwa hali hiyo licha ya kutishia maisha ya jamii,  pia ni mzigo kutokana na kulazimika kwenda mbali kufuatahuduma hizo.Mbunge huyo aliahidi kushirikiana na  Halmashauri ya Wilaya  kupitia mfuko wa jimbo kuhakikisha changamoto hizo  zinapatiwa ufumbuzi mara moja.Kwa upande wake, aliahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Pangani ili kuhakikisha kitengo cha upasuaji kinaimarishwa  haraka ili kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la kukosekana kwa hudumahiyo.Aweso alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Pangani kujiunga mfuko wa bima ya afya ili kupata matbabu kwa urahisi kwa kuwa kufanya hivyo kutapunguza gharama kwa wananchi wengi ambao wengi wao hawana uwezo wa kiuchumi.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa