Uhaba wa fedha wakwamisha miradi - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 28 Januari 2016

Uhaba wa fedha wakwamisha miradi

Serikali imesema kukosekana kwa fedha za kutosha kumechangia baadhi ya miradi ya maendeleo kusimama ikiwano ya barabara.Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, aliyetaka kujua ni lini serikali itapeleka fedha kwa mkandarasi  ili aweze kumaliza ujenzi wa daraja la Kilombero.Ngonyani alisema fedha za ujenzi wa daraja hilo zinatolewa na serikali kwa asilimia 100 lakini haiwezi kukamilisha miradi yote kwa wakati mmoja kutokana na uwezo wa mdogo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani.Alisema ujenzi wa daraja hilo unatarajia kukamilika Desemba mwakahuu.Akijibu swali la msingi lililohoji ni lini seriklai itaanza kumaliza ujenzi wa barabara ya Kidatu, Ifakara na Mlimba kwa kiwango cha lami.Alisema barabara ya Kidatu hadi Ifakara mradi huo umeanza kutekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na katika awamu ya kwanza naya pili jumla ya kilomita 16.17 zilijengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa