Rais wa John Magufuli amemwondoa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na kumteua kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.Katika mabadiliko hayo pia Magufuli amemwondoa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Clodwing Mtweve na kumteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, wateule hao wanakwenda kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.Tarifa hiyo ilisema Clodwing Mtweve amekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambayeuteuzi wake ulitenguliwa.Sefue alisema Chagonja anakwenda Katavi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa pia.Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Magufuli amewateua Makamishna hao wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.Makamishna Mtweve, Chagonja na Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa leo Jumamosi asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni