Baraza la Mawaziri EAC labanwa - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 31 Januari 2016

Baraza la Mawaziri EAC labanwa

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), wamelibana Baraza la Mawaziri wakihoji utekelezaji wa Mkataba wa Soko la Pamoja.Walichukua hatua jana katika vikao vya bunge vinavyoendelea jijini hapa, kutokana na hofu kuwa mchakato wa mtangamano unaweza kufikia mwisho bila masuala yanayohusu kazi na vibali vya makazi kupatiwa ufumbuzi.Akiwasilisha mchango wake bungeni humo, Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya, alielezea wasiwasi wa suala hilo kuwa sugu pasipoBaraza la Mawaziri kulizungumzia.“Hili suala limekuwa ni kibwagizo cha kila mwaka, wakati baadhi ya nchi zimeendelea kuongeza vibali vya kufanya kazi,” alisema.Alidai kuwa anatambua baadhi ya nchi wanachama zimejidhatiti kuifanya jumuiya hiyo ife.Wabunge hao walikuwa wakijibu ripoti ya maombi yaEALA kuhusu vibali vya kazi na makazi kwa raia wa nchi wanachama wa EAC kama ilivyowasilishwa bungeni hapo na mwenyekiti wake Dk. Odette Nyiramirimo kutoka Rwanda.Ripoti hiyo ilitayarishwa kwa pamoja na Chama cha Waajiri cha Afrika Mashariki (EAEO) na Umoja wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Afrika Mashariki (EATUC), Februari mwaka jana.Mapema mwaka huu, Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) lilimuomba Rais John Magufuli kuangalia upya suala la kupunguza bei ya vibali vya kazi na makazi kwa raia wa nchi wanachama wa jumuiya.Mbunge Susan Nakawuki kutoka Uganda, alizungumzia suala hilo akinukuu taarifa za vyombo vya habari kwamba imewarudisha makwao walimu waliokuwa wakifundisha nchini.“Kama tuhuma hizi ni za kweli basi hatujaanza wote kwa pamoja,” alisema.Kwa upande wake mbunge Hafsa Mossi kutoka Burundi alitoa changamoto kwa Baraza la Mawaziri akitaka kuweka kipaumbele suala la mkataba wa Soko la Pamoja katika vikao vya wakuu wa nchi vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.Mbunge kutoka Tanzania, Abdullah Mwinyi, alisema kuna umuhimu wa kubadili mtazamo miongoni mwa wanajumuiya kuhusu Soko la Pamoja.Akitoa majibu, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, Dk. Susan Kolimba, aliwahakikishia wabunge hao kwamba nchi wanachama italifanyia kazi suala hilo.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa