Mke wa Kafulila afufua Escrow bungeni - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 31 Januari 2016

Mke wa Kafulila afufua Escrow bungeni

Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Jesca Kishoa, amehoji kwa nini Tasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema watu 36 watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi lakini vinara wa kashfa ya Tegeta Escrow, ikiwa ni pamoja na Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Habirnder Seth Singh, hayumo.Kishowa ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye aliishupalia hoja hiyo bungeni na kuwang’oa baadhi ya vigogo wa serikali wakiwemo mawaziri.Kafulila ndiye Mbunge wa kwanza kuifikisha kashfa hiyo kwenye Bungeni la 10 na baadaye Ofisi ya Mdhimiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ikafanya uchunguzi na kuwasilisha ripoti yakeambayo ilifikishwa Bungeni na Kamati ya Hesabu za Serikali.Kashfa hiyo ilisababisha aliyekuwa Waziri wa Nishatina Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuachia ngazi.Watumishi wengine walioguswa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, Wenyeviti wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngelejana Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alikumbwa na fagio hilo.Kwenye mkutano wa jana wa Bunge, Kishowa alitakakupewa maelezo kwa nini mmliki huyo wa IPTL hajachukuliwa hatua na kusema hata baadhi ya maazimio ya Bunge yaliyopitishwa hayajafanyiwa kazi.Alisema ingawa anajua Mwenyekiti aliyekuwa akiongoza kikao cha jana, Chenge, ana maslahi katika suala hilo ni vyema akatoa mwongozo wa kiti.Akijibu mwongozo huo, Chenge alisema, limeulizwa sehemu ambapo siyo kabisa.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa