Kumefanyika maadhimisho ya kuwakumbuka watu walipoteza uhai wao kwenye ndege ya shirika la ndege la Malaysia
MH17, nchini Uholanzi,ambapo maua na mishumaa ipatayo mia mbili na
tisini na nane vilinavyo wakilisha idadi ya abiria waliokuwa wakisafiri
na ndege hiyo kabla ya ajali ambavyo viliwekwa na wanafunzi,ndege hiyo
ilipopotelea Mashariki mwa Ukraine yapata miezi minne iliyopita.
Mfalme na
malkia wa Uholanzi na mabalozi wa nje waliomo nchini humo walihudhuria
hafla hiyo,ambapo majina ya walikufa katika ajali hiyo yalitajwa.
Ikiwa
imetimia miezi minne leo, sababu za ajali hiyo mpaka sasa
hazijajulikana,ingawa kikundi cha kigaidi cha Urusi kinashukiwa
kuidungua ndege hiyo,ambayo ilikuwa ikifanya safari zake kutoka uwanja
wa ndege wa Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur Malaysia.
nasemekana ndege hiyo ilidunguliwa kwa kombora, na mara moja serikali mjini Moscow imekanusha taarifa hizo.bbc


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni