Miss Tanzania Happiness Watimanywa ambaye tayari kashafika jijini
Londoni kwa ajili ya mashindano hayo ya urembo kwa ngazi ya Dunia (Miss
World) amefanya mahojiano na mtangazaji wa kituo cha TV cha BBC SWAHILI
Salim Kikeke
tazama hapa
Kikeke alimuuliza Happiness juu ya vigezo vya msichana mrembo.."Mschana mrembo anatakiwa kuwa na vigezo gani?"
inategemea unamaanisha urembo gani? kwasababu kila mtu anakuwa na
tafsiri yake, kwenye mashindano kuna tafsiri nyingine kwa watu binafsi
kunakuwa kuna tafsiri nyingine. Mimi kama happiness Watimanywa najua
urembo ni kujivunia uzuri wako au vitu ambavyo umejaaliwa navyo lakini
ukienda sasa kwenye mashindano kunakuwa kuna tafsiri nyingine.
Salim: naweza kusema wewe ndio mshana mrembo kuliko wote Tanzania??
"sasa hiyo inategemea na nani anauliza au nani anadhani hivyo, kila mtu anakuwa na maoi yake".... alijibu happinesstazama hapa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni