Polisi nchini Italia wamemtia mbaroni mwanamme mmoja anayeshukiwa kumpiga hadi kufa mhamiaji mmoja raia wa Nigeria katika shambulizi la kibaguzi kwa misingi ya rangi.
Emmanuel Chidi amekuwa akiishi Italia tangu mwaka wa 2015, baada ya kutoroka vita nchini Nigeria.
Emmanuel Chidi alivamiwa siku ya jumanne alasiri katika mji Fermo alipokuwa akitembea na mkewe.Ripoti zinasema raia mmoja wa Italia alimtusi mkewe Chidi matusi ya kibaguzi .Matusi hayo yalichochea mvutano.Mwanamme huyo raia wa Italia kwa jina Amedeo Mancini baadaye alimshambulia Chidi kwa kutumia chuma.Chidi aliaga dunia siku moja baadaye.Maafisa wa polisi sasa wamemkamata mwanamme huyo na kumshtaki kwa makosa ya maauji yasio ya kukusudia, yaliyochochewa na ubaguzi wa rangi.
Mauaji hayo yamelaaniwa vikali kote nchini Italia.Waziri mkuu wa Italia bwana Matteo Renzi, amelaani vikali mauajihayo na kusema kuwa waitaliano wote wanapaswa kupinga ubaguzi wa rangi.
Wengi wanahofia kwamba huenda ikawa ishara ya taharuki inayotokana na wahamiaji wengi wanaopewa hifadhi nchini humo kutoka barani Afrika.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Alhamisi, 7 Julai 2016

Home
Unlabelled
Ubaguzi wa rangi: Mnigeria auawa Italia
Ubaguzi wa rangi: Mnigeria auawa Italia
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni