Makosa matatu ya Nay wa Mitego yaliyofanya afungiwe na BASATA kwa muda usiojulikana,yafahamu hapa.. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 28 Julai 2016

Makosa matatu ya Nay wa Mitego yaliyofanya afungiwe na BASATA kwa muda usiojulikana,yafahamu hapa..

Siku chache baada ya baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kuufungia wimbo wa Nay wa Mitego ‘Pale kati Patamu’,siku ya leo baraza hilo limetangaza kumfungia msanii huyo kujihusisha na shughuli za muziki kwa muda usiojulikana mpaka watakapojiridhisha kuwa rapper huyo amefuata vigezo walivyotaka avifuate.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey L. Mngereza, imemtaka rapper huyo kulipa faini ya shilingi milioni 1, na kufanya marekebisho ya mashairi ya wimbo wake wa ‘Pale Kati’, kufuata sheria, kanuni na taratibu za urasimishaji sekta ya Sanaa kwa maana ya kusajiliwa na BASATA na kuhakikisha wimbo wake umefuata taratibu zote.

Pia, ameagizwa kuwaomba radhi watanzania kwa kutoa kazi ya muziki yenye kuvunja maadili na kudhalilisha watu wa kada mbalimbali hususani wanawake

.Maamuzi hayo yamefanyika kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) cha sheria nambari 23 ya mwaka 1984, ikisomwa pamoja na kifungu cha30(1)(2) na waraka wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo wa tarehe 16/7/2009 ambayo kwa sasa inafahamika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Adhabu hizo zimetolewa baada ya BASATA kufanya kikao cha pamoja na msanii huyo siku ya jana.

Makosa aliyosomewa na yeye kuyakiri kwa maandishi ni pamoja na;

1. Kujihusisha na shughuli za Sanaa pasipo kusajiliwa na BASATA.

2. Kutoa wimbo wa “Pale Kati” na kuupakia katika mitandao ya kijamii bila kuuleta kufanyiwa uhakiki wa maudhui yake.

3. Maudhui ya wimbo wa ‘Pale Kati’ kwa sehemu kubwa hayafai kwamatumizi ya wazi na ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya mtanzania.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa