Wataka utendaji wake upimwe baada ya miaka mitatu. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumanne, 29 Machi 2016

Wataka utendaji wake upimwe baada ya miaka mitatu.

Wakati Rais John Magufuli, leo anatimiza siku 146 akiwa Ikulu tangu alipoapishwa Novemba 5, mwaka jana, mtindo wake wa kupangua wakuu wa mashirika na  idara za serikali unaowakosesha usingizi vigogo, umetafsiriwa na wasomi kwamba ni njia ya kupanga kikosi chake na kwamba ni vyema akaanza kupimwa baada ya miaka mitatu.Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, amekuwa akifanya mabadiliko kwa watendaji wake kwa staili ya kipekee, tofauti na utaratibu uliokuwa unafanywa na watangulizi wake.Rais mstaafu, Jakaya Kikwete wakati wa utawala wake, alifanya mabadiliko makubwa ya mawaziri mara tatu na madogo mengine mara tatu kwa kuwabadilisha mawaziri kutokana na sababu mbalimbali.Mabadiliko ya kwanza makubwa ya Baraza la Mawaziri yalikuwa mwaka 2008, yaliyotokana na kashfa ya mkataba wa Richmond na mwaka 2012 lifanya mabadiliko mengine kutokana na kashfa iliyotokana na ripoti ya CAG, huku mwaka 2014 akifanya mabadiliko tena kutokana na kashfa ya Operesheni Tokomeza Ujangili.Hali hiyo imekuwa tofauti kwa Rais Dk. Magufuli, ambaye amekuwa akifanya mabadiliko taratibu kwa mtumishi mmoja mmoja pindi anapoona hafai au hastahili kuwapo katika nafasi hiyo.MABADILIKO YA RAIS MAGUFULIItakumbukwa Desemba 20, mwaka jana, Rais Magufuli alimteua Eliakim Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), uteuzi uliodumu kwa siku 32 tu hadi Januari 20, mwaka huu,  na kuamishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya mawasiliano Ikulu ilieleza kuwa Rais Magufuli alimwondoa Maswi TRA baada ya kukamilisha kazi maalum aliyomtuma kuifanya.Aliyekuwa Katibu MKuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema Rais Magufuli alifanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na Maswi.Kadhalika, Desemba 20, mwaka jana, Rais Magufuli pia alimteua Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu MkuuKiongozi Ikulu, nafasi aliyodumu nayo kwa siku 78 tu.Uteuzi huo ulitenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi John Kijazi. Wakati wa kuteungua uteuzi huo, Machi 6, mwaka huu, ilielezwa kuwa Balozi Sefue atapangiwa kazi nyingine.Vile vile Rais Dk. Magufuli wakati akitangaza Baraza lake la Mawaziri Desemba 10, mwaka jana, alimteua Prof. Makame Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, nafasi aliyodumu nayo kwa siku 13 hadiDesemba 23, alipombadilisha na kumpeleka katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Nafas  yake ilijazwa na Mhandisi Gerson Lwenge.Rais Dk. Magufuli hakuishia hapo kwani Desemba 7, mwaka jana, alifanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi nchini kwa kumhamisha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, kumpeleka kuwa Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.Nafasi ya uteuzi huo, ilidumu kwa siku 54, alipohamishwa tena na kuteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Januari 29, mwaka huu.Mabadiliko mengine yaliyofanyika ni utenguzi wa nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Carina Wangwe, aliyeteuliwa Machi 3, mwaka huu, na Waziriwa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, kabla ya kutenguliwa siku hiyo hiyo.WASOMI WANASEMAJEMhadhiri wa  Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma katika  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Bashiru Ally, alisema Rais Magufuli hana muda maalum wa kufanya mabadiliko ya kiutendaji kwa watumishi wa serikali.Alisema Rais Magufuli ni tofauti na Bunge au uteuzi wa chama ambao mtu akishachaguliwa kuondoka kwake hadi muda wake umalizike.“Hawa ni watendaji, hawana muda maalum, muda wowote wanahamishwa au kufukuzwa, hivyo Rais Magufuli anafanya kwa mujibu wa katiba inayompa nguvu,” alisema Ally.Alisema mtendaji anaweza kuteuliwa muda wowote na kuondolewa muda wowote atakao rais, hivyo inawezekana mtu akateuliwa na kukaa muda mrefu katika nafasi hiyo.“Kwa mfano, Dau amekaa NSSF zaidi ya miaka 10 tangu utawala wa Rais Mkapa, Sumaye amekaa miaka 10, Katibu Mkuu (Patrick) Rutabanzibwa a alikaa muda mrefu sana, wakuu wa majeshi nao wanakaa muda mrefu, lakini siku rais akiona ana haja ya kubadilisha, anaamua muda wowote,” alisema.Naye Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Israel Sosthenes, alisema mabadiliko anayoyafanya Rais Magufuli si mabaya, na ni mambo ya kawaida kwa rais yeyote.Alisema hali hiyo ni ya mpito na itatulia kwa sababu Rais Magufuli bado anaimarisha safu ya watendaji katika serikali yake.“Ni sawa sawa na kocha mpya wa mpira wa miguu, amepewa timu mpya, hivyo anawajaribu wachezaji wake kwa kuona yupi anafaa, yupi hafai. Itafikia wakati kocha atapata timu nzuri ya ushindi aitakayo,” alisema Sosthenes.Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, alisema Rais Magufuli kufanya mabadiliko hayo ni katika jitihada za kujipanga kiutendaji na kuweka safu vizuri.Alisema Rais Magufuli bado anapanga watendaji wake, hivyo ana wajibu wa kumtoa mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.“Yeye ndiye anayewahitaji. Anaweza kuweka mtu sehemu na kumtoa muda wowote, hivyo bado anajipanga,” alisema Nghwira.Mchambuzi wa masuala ya siasa, Abdulhakim Atiki, alisema Rais Magufuli anapaswa kupewa muda wa miaka mitatu wa tathimini wa haya anayoyafanya.“Unapoingia katika nafasi ya uongozi kama ya urais, unajaribu kupata 'tune' (sauti) ya jambo fulani, unajaribu kuweka kitu hapa kule, hadi pale utakapopata 'tune' nzuri, na ndicho anachofanya Rais Magufuli,” alisema Atiki.Alisema kwa sasa Rais Magufuli ana haki ya kutafuta namna ambayo anawajaribu watendaji wake, hivyo ana falsafa yake ya utendaji.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa