Magufuli akabidhiwa rungu kuwamaliza watafuna nchi - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumanne, 29 Machi 2016

Magufuli akabidhiwa rungu kuwamaliza watafuna nchi

Ni ripoti ya CAG ya mwaka wa mwisho wa Rais Kikwete, PAC yasema hatapepesa macho wala kumwonea mtu aibu�


Wakati Rais John Magufuli akiwasimamisha kazi takriban watumishi 200 wa umma kutokana na kashfa mbalimbali zilizosababishia serikali kupoteza mabilioni ya fedha, jana Mbidhiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, alimkabidhi ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka 2014/15.Kupitia ripoti hiyo, watumishi wa umma ambao watabainika kuhusika na ubadhirifu wa mali ya umma, watashughulikiwa ipasavyo kwa kuchukuliwambalimbali zikiwamo kufukuzwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sharia.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),  Aesh Hilary, ameiambia Nipashe kwamba wakishakabidhiwa ripoti hiyo na rais, watahakikisha wanatekeleza majukumu yao bila kumwonea mtu aibu.Ripoti hiyo, ambayo kimsingi inahusu hesabu za serikali kuu, serikali za mitaa na mashirika ya umma,wakati wa Rais Jakaya Kikwete, inatoa fursa kwa Rais Magufuli kuendelea kufumua idara na mashirikaambayo kila mara yamekuwa yakiainishwa na CAG kuwa kuwa ni kichochoro cha ukwepaji kodi na ufujaji wa fedha.Tangu Rais Magufuli aapishwe Novemba 5, mwaka jana, amewasimamisha na kuwafukuza kazi maofisawa serikali na kuvunja bodi mbalimbali, hali iliyosababisha takribani watu 200 kukosa kazi.Hali hiyo imekuwa ikitafsiriwa kwamba ni kuonyeshaudhaifu wa serikali iliyopita, jambo ambalo sasa linatarajiwa kuongezeka baada kuwekwa wazi kwa ripoti ya CAG, inayoishia Juni 2014.Moja ya maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikubwa ni Mamlaka ya Bandari (TPA). Katika mamlaka hiyo, baadhi ya maofisa wake wamesimamishwa kwazi kutokana na makontena kuondolewa bandari ya Dar es Salaam bila kulipigwatozo ya bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Taarifa ya IkuluTaarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, inasema Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi.Ilisema baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuliataikabidhi mbele ya bunge katika siku saba za mwanzo za mkutano ujao wa Bunge, unaotarajiwa  kufanyika mjini Dodoma.“Rais Magufuli amempongeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo, na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” ilisema taarifa hiyo.PACAkizungumza na gazeti hili, Hilary ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa PAC, alisema anaamini serikali ya Rais Magufuli iliyojipambanua kwamba inachukia rushwa, itatekeleza ushauri wote wa kamati hiyo baada ya kuchambua ripoti hiyo.“Tutaitendea haki ripoti na kama kuna upungufu tutakuwa wazi. Kama  kuna ubadhirifu tutasema bila kupepesa macho.“Tunaamini tukimshauri rais atafanya kazi. Naamini  maazimio ya Bunge yataheshimiwa kwa sababu kaziyake ni kuishauri na kuisimamia serikali,  sasa hivi tunangoja rais atuletee hiyo ripoti,” alisema.Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 2014Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 2014, ilihusisha ukaguziwa taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109.Ripoti hiyo iliainisha kwamba, madeni ya Wizara ya ujenzi iliyokuwa chini ya Dk Magufuli, yalikuwa Sh. bilioni 800, ukwepaji kodi Sh. bilioni 800, malipo yaliyofanyika bila kutolewa stakabadhi Sh. bilioni 4.6.Mishahara hewa ilikuwa Sh. bilioni 141.4 ufujaji miradi ya maendeleo. Sh. bilioni 312 misamaha ya kodi migodini na Sh. bilioni 22.33 madeni mifuko ya jamii.Profesa Assad alisema pia kuwa Sh. milioni 543 zilizotumika kulipa posho ya pango nje ya nchi kwa watumishi waliokuwa wakifanya kazi kwenye balozi mbalimbali wakati walikuwa wameshastaafu.Ripoti hiyo ilibaini ukiukwaji wa matumizi ya utoaji wa misamaha ya kodi, kuendelea kwa mishahara hewa, usimamizi mbovu wa mipango miji, madeni ya serikali katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).Kwa mujibu wa ripoti hiyo, misamaha ya kodi kwa mafuta yanayotumika migodini imefikia Sh. bilioni 22.33 kati ya yale yaliyotakiwa kutumiwa na kampuniza Geita Gold Mine na Resolute Tanzania Ltd, lakini yalipelekwa kwa makandarasi wasiostahili.Alisema amebaini kudorora kwa uwekezaji wa serikali kwenye kampuni mbalimbali, ambako serikaliina hisa kutokana na kuchelewa kuongeza mtaji, wakati inapohitajika kufanya hivyo kama ambavyo inataka kutokea katika benki ya NBC Ltd.Mashirika ambayo yamegubikwa na kusuasua kwa usimamizi wa uwekezaji wa serikali ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ambayo yote yanahitaji ruzuku kutoka serikalini.Ripoti hiyo ilibaini kwamba wafanyabiashara wengi kutotumia mashine za kielektroniki za kutolea stakabadhi, kuliisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 4.4.Ukaguzi wa CAG umebaini wafanyakazi walioacha kazi na kustaafu wameendelea kulipwa na kiasi kilichokuwa kimetumika kwa mwaka huo kilikuwa Sh. milioni 141.4.Alisema katika halmashauri 36, Sh. bilioni 1.01 zililipwa kwa watumishi waliotoroka kazini.Ripoti hiyo iliitaja Wizara ya Ujenzi iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Magufuli kuwa inaongoza kwa kudaiwa na makandarasi.Alisema mpaka anatoa ripoti hiyo, wizara hiyo ilikuwa ikidaiwa Sh. bilioni 800 na kwamba mpaka wakati huo ilishatumia Sh. bilioni 250 nje ya bajeti husika.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa