Serikali imetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wazazi na walezi wa wanafunzi juu ya mpango wa utoaji elimu bure kwa shule za msingi na sekondari nchini, ili kukabiliana na changamoto ya wazazi kukwepa majukumu yao.Wito huo ulitolewa na walimu 112 wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Nachingwea, wakati wa mahafali yao ya kuhitimu mafunzo ya ufundishaji, ujifunzaji na tathimini yaliyotolewa na mradi wa kuimarisha na kuboresha mifumo ya elimu, Afrika ya Mashariki (Sesea) unaotolewa na Chuo Cha Aga khan kwa ufadhili wa serikali ya Canada.Mwalimu wa Shule ya Msingi Mandai, Salma Nahonyo alisema wamekuwa wakikutana na changamoto ya wazazi kugoma kuwanunulia watoto wao sare za shule kwa madai kuwa serikali imetangaza elimu bure."Wazazi na walezi bado hawana elimu ya kutosha juu ya elimu bure," alisema Nahonyo."Hasa huku vijijini wanaamini mtoto wake atapata huduma zote shuleni ikiwamo madaftari, kalamu na mavazi hali ambayo inatuwia ngumu kuwaelimisha na kudhani walimu tunapingana na agizo la serikali."Alisema serikali inapaswa kutoa elimu na kuahinishamahitaji ambayo wazazi wanapaswa kuyachangia ili kuondokana na migongano ya kudhani walimu wanataka kuwaibia wazazi.Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mitumbati, Mashamu Kienula alisema wazazi hawatambui thamani ya elimu hivyo wamekuwa wagumu kushiriki kukagua maendeleo ya watoto wao pamoja na kukwepa majukumu ya kuwaanunulia vifaa vya shule."Wazazi wa wilaya hii hawana ushirikiano na walimuna wanafunzi... wanakwepa kutimiza majukumu yao hali inayowafanya walimu nao kufanya kazi kwenye mazingira magumu," alisema.Alisema wanafunzi wanategemea uangalizi wa walimu pekee huku wazazi wakiwafanyisha kazi za nyumbani bila kuwasikiliza kimasomo.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa wilaya ya Nachingwea, Mhandisi Jakson Masaka, alisema pamoja na changamoto za wazazi kuwa wagumu kuelewa mpango wa elimu bure pia wamekuwa si wafuatiliaji wa maendeleo ya watoto wao pindi wanaporudi nyumbani hali inayosababisha mahudhurio kushuka.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni