Majambazi matatu yameua watu wawili na kujeruhi wengine saba kwa risasi wakati yakipora maeneo ya Bugarika Sokoni, kata ya Pamba wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza juzi usiku.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Yustus Kamugisha, alisema mauaji hayo yalitokea saa 2:05 usiku katika eneo hilo.Alisema majambazi hayo yalikuwa na bunduki aina ya SMG au SAR, na yalivamia duka la Daniel Marwa mkazi wa Bugarika na kufanya uporaji huo.Kamanda Kamugisha aliwataja waliouawa ni mwendesha bodaboda Julius Wankaba mkazi wa Bugarika na mwanamke mmoja, Mama Yuni aliyepigwa risasi ya shingo wakati akikimbia toka dukani kwake.“Wakati wanaingia eneo la tukio, wahalifu hao walianza kufyatua risasi hovyo,” alisema Kamugisha,"kabla ya kufanya uporaji katika duka la Marwa linalojishughulisha na huduma ya pesa na kupora Sh. milioni 2 na vocha zenye thamani ya zaidi ya Sh. 800,000."Alisema baada ya kufanya mauaji hayo, majambazi hao waliwafyatulia risasi watu wengine saba ambao watano kati yao wamelazwa hospitali ya Rufaa Bugando na wawili hospitali ya mkoa, Sekou Toure.Kamugisha aliwataja waliojeruhiwa ni Magesa Mungari ambaye ni dereva wa bodaboda na Simon Charles ambao wamelazwa Sekou Toure.Wenigne ni Mwita Ryoba, Frank Willium, Saumu Said,Masumbuko Kanduru na Emmanuel Francis, wote wakiwa wamelazwa Bugando.Jeshi la polisi linaendesha msako mkali wa kuwasaka watu hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka yatakayowakabili, alisema.Katika tukio jingine, mwanamke mmoja asiyefahamika, aliingia hospitali ya wilaya ya Magu na kuiba mtoto wa siku moja, Kamanda Kamugisha alisema.Alisema mwanamke huyo aliyevuka geti la hospitali hiyo akiwa amevaa ushungi, aliingia ndani ya wodi aliyokuwa mama mzazi, Madgalena Petro, aliyejifungua mtoto wa kike wa siku moja.Baada ya kumkuta mzazi huyo amelala, alimchukua mtoto huyo na kutoweka naye, alisema.“Alipoamka hakuweza kumuona mtoto wake, hivyo kutoa taarifa kwa wauguzi ambao walianza kumtafuta bila mafanikio,” alisema Kamugisha."Polisi tunawashikilia baadhi ya wauguzi, madaktari na walinzi."
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni