Serikali yaja na kisingizio cha kuibiwa walimu. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 5 Machi 2016

Serikali yaja na kisingizio cha kuibiwa walimu.

Serikali  imekiri udhaifu kwa shule zake kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa, huku ikijitetea kuwa za binafsi zinafanya vyema kwa sababu zinaiba walimu waliosomeshwa na serikali na kuwalipa fedha nyingi.Kauli hiyo ya serikali imetolewa wiki chache baada ya Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (Necta), kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. uliofanyika Novemba. mwaka jana. huku shule zzakezikifanya vibaya kuulinganisha na za binafsi.Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Eustella Bhalalusesa, alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa  akizungumza na Nipashe. Gazeti hili lilitaka kujua sababu ya shule za serikali kufanya vibaya.Prof. Bhalalusesa alisema sababu ya walimu hao kushawishika na kukubali kwenda kufundisha shule binafsi, ni kutokana na  mishahara wanayolipwa kuwa mikubwa na kwamba serikali haiwezi kuimudu.Wakati kamishna huyo akieleza hayo, matokeo ya kidato cha nne yaliyotangwaza wiki mbili zilizopita, yanaonesha shule za serikali zimeendelea kushika mkia.Katika matokeo hayo, shule za serikali ambazo ni za watoto wenye vipaji maalumu zilizokuwa zimezoeleka kufanya vizuri, hazikufua dafu kutokanana Ilboru kushika nafasi ya 53, Kibaha (69), Mzumbe (71) na Kilakala nafasi ya 94.“Hawa wenzetu wamewekeza na unakuta ada ya mtoto mmoja pekee ni Sh. milioni tisa sasa unafikiri watashindwaje kumchukua mwalimu kutoka serikalini pindi wanapomtaka? Walimu tunaobakia nao ni wazalendo pekee,” alisema.Prof. Bhalalusesa alisema sababu nyingine ni shule za serikali kuchukua wanafunzi wa kawaida wakati za binafsi huchukua walio bora.Alisema wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza shule za serikali na wale wa binafsi wanatofautiana, ndiyo maana matokeo yanapotoka wao hufanya vizuri zaidi.“Ila kwa kidato cha sita, matokeo huwa tofauti kwa sababu hawa tayari wamechujwa na mitihani ya kidato cha nne, kwa hiyo ufaulu wao huwa mzuri zaidi,” alisema.Kuhusu mikakati ya serikali katika kuziboresha shulehizo, Prof. Bhalalusesa alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2016/17, baadhi ya shule hizo zitakarabatiwa.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa