Mahakama: Kubenea ana kesi ya kujibu. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 5 Machi 2016

Mahakama: Kubenea ana kesi ya kujibu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea, ana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma za  kutoa lugha ya matusi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri.Hakimu Simba alisema ushahidi uliotolewa unaonyesha maswali dhidi ya mshtakiwa na kwamba anatakiwa kupanda kizimbani kujitetea.Alisema ushahidi wa upande wa utetezi utaanza kusikilizwa Machi 7, mwaka huu.Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema upande wake unatarajia kuita mashahidi wanne akiwamo mshtakiwa.Hakimu Simba alisema dhamana ya mshtakiwa inaendelea na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa ushahidi wa utetezi Machi 7, mwaka huu.Katika kesi ya msingi, Kubenea anadaiwa kuwa Desemba 14, mwaka jana, katika Kiwanda cha Tooku Garments kilichoko maeneo ya Mabibo External wilayani Kinondoni, Kubenea alitumia lugha ya matusi dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda, hali ambayo ingesababisha uvunjifu wa amani.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa