Msanii aliyefanya vizuri na ngoma kibao kali PNC amefunguka na kusema kwake yeye hawezi kuendelea kukaa kimya kwenye muziki kwa kuwa hana uongozi unao msimamia kazi zake, amedai ataendelea kufanya kazi ya muziki na kutoa kazi kwakukomaa mwenyewe
Kwani muziki kwake umemuingia sana mwilini kamamadawa ya kulevya na kusema hawezi kuacha muziki.PNC akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alidai kuwa yeye muziki ni kitu anachokipenda licha ya kuwa ni kazi inayomuingizia kipato hivyo hawezui kuacha bali atakuwa anakomaa na kufanya sababu muziki yeye umemuingia kama madawa ya kulevya hivyo umemuingia sana mwilini na kuacha hawezi."Mimi sina management kwa hiyo siwezi kusema niache kutoa kazi, kwangu muziki naupenda tukiachamuziki kama kazi kuwa unaniingizia kitu. Ni kweli sina uongozi wowote ila kila kitu nafanya mwenyewe,nakomaa mwenyewe yaani muziki kwangu ni kama madawa ya kulevya yameniingia sana mwilini hivyo siwezi kuuacha, bado sijapata management hivyo navyojisikia kufanya kazi nafanya, nakomaa kwa nguvu zangu na niwahakikishie kuwa ngoma yangu ya Ekotite nafanya bonge moja ya video na watu watakubali na kuelewa na watasema kweli nafanya kitu" amesema PNC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni