Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, amemtaka Mtendaji Mkuuwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo itaonyesha idadi ya nyumba za serikali wanazomiliki na kubainisha taarifa ya watumishi wenye stahili ya kupangishwa kwenye nyumba hizo.Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ilieleza kuwa Ngonyani alitoa agizo hilo alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini ya wizara ikiwamo TBA.Taasisi zingine alizozitembelea ni Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC). Lengo la ziara hizo lilikuwa kupata mafunzo ya kiutendaji katika taasisi hizo.Katika ziara hiyo, Ngonyani alizitaka taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya mapato zilizo navyo badala ya kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.“Nataka ifikapo mwaka wa fedha ujao, makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi kuliko matumizi na kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka serikalini. Kikubwa ni kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kujiendesha”, alisema.Pia Naibu Waziri Ngonyani aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na bila woga kwa kuwa serikali haitamwonea huruma yeyote anayekiuka kutekeleza wajibu wake.Kadhalika, Mhandisi Ngonyani alimtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole Kujan, kutatua changamoto walizo nazo ili kuleta mabadiliko chanya katika taasisi hiyo.Naye ole Kujan alisema Temesa imejipanga kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini na kuhakikisha inapunguza changamoto ya usafiri katika vivuko.Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Mhandisi Julius Mamilo, alibainisha changamoto walizo nazo ikiwamo uhaba wa fedha, hali inayosababisha baraza kukwama katika kufanya kazi katika miradi yake ya maendeleo hususani katika kufanya kazi za utafiti.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni