Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rudani ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula, kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000.Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia jana na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Alfred Luanda, asimamie utekelezaji wa agizo hilo mara moja.Majaliwa alitoa agizo hilo jana, kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo, alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa waliolazwa.Baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda moja kwa moja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokea wagonjwa wote."Dirisha la wazee lipo?" akajibiwa hakuna. "Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo?" nalo pia akajibiwa halipo. "Je wazee wana daktari wao?", hakupata jibu.Baada ya kushindwa kupata majibu ya maswali hayo, aliuliza: "Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee na uhakikishe wana daktari lao. Si kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana."Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa na ndugu wa wagonjwa waliokuwa wakiimba "tuna jambo, tuna jambo" wakiashiria kutaka kusikilizwa.Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuualipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei ya juu kwenye maduka ya watu binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.Lakini kero ya Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake, lenye ukubwa wa ekari 2.5, ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula, ndiyo ilimgusazaidi Waziri Mkuu."Februari Mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za Sh. 85,000 hapo nje,pia uzi wa kushonea kwa Sh. 25,000. Lakini pia daktari akasema anataka Sh. 100,000 ya kwake. Lakini hadi Februari 7, hakufanyiwa huo upasuaji."Tarehe 12 Februari baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetuKilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000 na babaakafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani."Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?" alisema.Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza.Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya kinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.Akiwa njiani kwenda chumba cha upasuaji, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi ulifanyika jana waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo.Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika."Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC (Kamanda wa Polisi wa Mkoa) hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho," alisema.Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu alimwagiza RAS, Mganga Mkuu wa Mkoa na Ofisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wotewa hospitali hiyo jana saa tisa alasiri na kisha wampelekee letee taarifa.Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu, hivyo wanapaswa kuwa na huruma na si kuwaumiza wananchi wa kipato chachini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama zamatibabu.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni