Mbunge Pauline Gekul afunguka - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumanne, 29 Machi 2016

Mbunge Pauline Gekul afunguka

Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul, amejikuta atika wakati mgumu baada ya kuuziwa nyumba yenye utata na hatimaye vifaa vilivyokuwa ndani kutupwa nje juzi jioni.Vifaa hivyo vilitupwa nje ikiwa ni utekelezaji wa amri ya mahakama kwa kuwa mmiliki wa nyumba hiyo alikuwa akidaiwa.Akizungumza na Nipashe jana, Gekul alisema nyumba hiyo alikuwa amempangisha mpangaji wakati vifaa hivyo vilipotupwa nje.Alisema alikuwa hajui kama alikuwa amenunua nyumba hiyo kutoka kwa mtu mmoja ambaye alikuwa akidaiwa na benki mbili za CRDB na NMB.Mapema, baada ya kutupiwa vitu nje juzi jioni, Pauline ambaye yuko safarini nje ya mji wa Babati, alisema kwa simu kuwa hadaiwi na taasisi yoyote yafedha na kwamba hajatupiwa vifaa nje.Alisema baada ya kununua nyumba hiyo alimpangisha mtu mmoja, ambaye ndiye vifaa vyake vilitolewa nje.Mkazi mmoja jirani na nyumbani hapo, alisema jana kuwa taarifa zilizoenea mitaani ni kwamba nyumba hiyo ilikuwa ikidaiwa na benki.“Kwa taarifa ninazozisikia mitaani ni kwamba mbunge amenunua nyumba kutoka kwa mtu ambayealikopa CRDB na NMB, lakini waliokuwa na hali halisi ni CRDB, “ alisema mkazi mmoja.Nipashe ilipofika nyumbani hapo eneo la Sido, ilimkuta mlinzi ambaye hakuwa tayari kuzungumza badala yake alimpigia simu bosi wake ambaye aliiambia Nipashe wao hawamjui mmiliki.Mlinzi huyo alisema ofisi yake ilipewa kazi na benki ya CRDB kulinda nyumba hiyo.Mwenyekiti wa Mtaa wa Negamsi,  Wiston Mkanwa, anayeishi jirani na nyumba hiyo, alikiri kutokea tukio hilo, ambalo alisema aliitwa na mwanasheria wa  CRDB kwa ajili ya kwenda kusimamia kuvunjwa milango na kutoa vitu na baadaye alisatia saini kaeratasi iliyoonyesha vitu vilivyotolewa.Akizungumza zaidi Pauline alisema alianza kuimiliki nyumba hiyo Januari mwaka huu, akiwa na hatimilikihalali.Kwa upande wake, Meneja wa CRDB,  Ronald Paul, alisema wao hawamjui mbunge huyo kuwa ndiye mmiliki bali wanamtafuta mpangaji wa nyumba hiyo.Alipotafutwa meneja wa NMB hakuweza kupatikana kwenye simu yake ya mkononi.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa