Rais Dk. John Magufuli, jana alimwapisha Mkuu wa mkoa mpya wa Songwe, Chiku Gallawa, ambaye hakuapishwa pamoja na wakuu wa mikoa wenzake, Machi 15, mwaka huu.Taarifa iliyotolewa na kaimu Mkurugwenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, ilisema hafla hiyo ilifanyika jana Ikulu Jijini Dar es salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.Gallawa anakuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza Songwe, ulioanzishwa kwa kuugawa mkoa wa Mbeya, Kusini mwa Tanzania.Wakati huo huo, Rais Dk. Magufuli jana alipokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali yza mwaka 2014/2015 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Rais Magufuli alipokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa Machi.Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli ataikabidhi mbele ya bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge kitakachofanyika mjini Dodoma.Rais Magufuli alimpongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na kutoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni