Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza, amesema juhudi za utendaji kazi katika awamu ya tano, zinatakiwa zifanywe na watendaji wote badala ya kumwachia Rais John Magufuli pekee.Mchungaji Lwiza alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana, muda mfupi baada ya ibada ya Jumatatu ya Pasaka, katika Kanisa la Kuu la Azania Front, Dar es Salaam.Alisema katika kipindi kifupi cha serikali ya awamu hiyo, kumekuwa na juhudi mbalimbali ambazo zimefanyika, ikiwamo kurudisha nidhamu kazini. Hata hivyo, Mchungaji Lwiza alisema juhudi hizo zimeonekana kufanywa zaidi na Rais pekee.“Tunashukuru kwamba serikali ya awamu hii imeanza kurejesha nidhamu kazini ambayo ilianza kupotea, ikiwamo kuwataka watu wawajibike na kuheshimu kazi wanayopewa. Lakini tunaona juhudi hizi zilizofanywa kwa kipindi kifupi bado watendaji wengine hawajawajibika vya kutosha, isipokuwa kazikubwa inafanywa na Rais,” alisema.Aliongeza kuwa: “Juhudi hizi zinapaswa kufanywa pia na watendaji wengine na si kumwachia Rais pekee kwa sababu safari yake bado ni ndefu, bila kusaidiwa na watendaji wengine anaweza kuchoka.”Kuhusu hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa na serikali hiyo, maarufu kama ‘kutumbua majipu’, Mchungaji Lwiza alisema ni nzuri isipokuwa serikali inapaswa kuhakikisha inazingatia haki pasipo kumwonea mtu.“Kuwachukulia watumishi hatua pale wanapokosea au kuzembea si kitu kibaya, lakini jambo ambalo linatakiwa kuzingatiwa ni kutokumwonea mtu na kuhakikisha serikali inafanya hivyo kwa kuzingatia sharia. Kwa yule anayebainika hana hatia arejeshwe kazini,” alisema.Pia alisema jambo lingine ambalo linapaswa kupongezwa katika serikali ya awamu ya tano ni ukukusanyaji wa mapato tofauti na vipindi vingine vilivyopita.Alisema kusimamia vyema katika kipengele hicho kutasaidia kupunguza umaskini kwa wananchi wake kwa kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya maendeleo.Mchungaji Lwiza alisema kutokana na juhudi zinazofanywa na Rais, iko haja kwa viongozi wa dini kuendelea kumwombea ili aendelee kutekeleza majukumu ambayo ameyaanza na kwamba anaamini kwamba mtu yeyote anayesimamia haki hawezi kukosa maadui.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni