Jaji Ramadhani kuongoza jopo la majaji kesi ya Babu Seya - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatano, 2 Machi 2016

Jaji Ramadhani kuongoza jopo la majaji kesi ya Babu Seya

Baada mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanae, Johnson Nguza(Papii Kocha), kushindwa Mahakama ya Rufani na kukimbilia Mahakama ya Haki za Binadamu na Watu ya Afrika (AFCPHR), sasa shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa Machi 11.Ratiba ya shughuli zitakazofanyika mahakamani hapo katika vikao vyake vya kawaida, zinaonyesha kuwa Rais wa mahakama hiyo, Jaji Agustino Ramadhani, tayari amekwishaanza kuongoza vikao vya majaji wenzake kusikiliza kesi mbalimbali zaidi ya 50.Kesi ya Babu Seya ni miongoni mwa kesi zilizopangwa kusikilizwa Machi 11, mwaka huu.Mahakama hiyo ina majaji 11 kutoka nchi wanachama wa umoja wa Afrika (AU) ambapo hukutana mara nne kwa mwaka katika vikao vyake vya kawaida.Walalamikaji hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya kumlazimisha malalamikiwa (Serikali ya Tanzania) kuwaachilia huru, kulipwa fidia na nafuu zingine ambazo itaona kuwa wanastahili kuzipata.Katika shauri hilo namba 006/2015, walalamikaji wanaiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi kwamba haki zao zimevunjwa na hivyo waachiwe huru na kulipwa fidia.Aidha wameiomba mahakama hiyo kuwawezesha kupata uwakilishi au msaada wa kisheria na pia iteue wataalam kutoa ufafanuzi wa hoja za kesi na kuisaidia mahakama iweze kufikia utekelazaji wa wajibu wake.Kwa mujibu wa walalamikaji, mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki.Mathalan wamedai, hati ya mashtaka yao ilikosa kuandikwa tarehe ya siku tuhuma za makosa yalipodaiwa kufanywa, hali ambayo iliwafanya washindwe kutayarisha utetezi.Pia walidai mahakama iliyowatia hatiani, ilizingatia ushahidi wa upande wa mashtaka usioshirikisha ushahidi mwingine.Walidai Serikali ya Tanzania kupitia maafisa wake, walivunja misingi yote ya haki za binadamu na sheria za kimataifa.Walidai mlalamikiwa alivunja Ibara 1,2, 3, 5, 7(1)b), 13 na 18(1) ya Chata ya Afrika kuhusu Ubindamu na Haki za Binadamu.Walidai kuwa baada ya kukamatwa, hawakuelezwa mapema kuhusu mashtakawaliyokuwa wakituhumiwa nayo na hivyo kuwekwa chini ya ulinzi kwa siku nne bila kuwa na mawasiliano na kupata fursa ya kuonana na mwanasheria au mtu mwingine yeyote.Wakiwa chini ya ulinzi, walidai polisi waliwatesa ikiwa ni pamoja na kuwatukana. Walisema baada ya kuwa chini ya ulinzi kwa muda huo wote, ndipo afisa mmoja wa polisi alipowaeleza kuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji.Kwa mujibu wa walalakaji, shauri lao halikutendewa haki kwa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na mahakama kutupilia mbali maombi yao ya kuwasilisha ushahidi wa vipimo vya damu na mkojo.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa