Tangazo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwamba walimu watakuwa wakisafiri bure kwenye mabasi ya daladala mkoani Dar es Salaam, utekelezaji wake unaelekea kuwa mgumu.Wakati hali hiyo ikionekana hivyo, Chama cha Walimu nchini (CWT) kimesema kinahitaji kuwapo kwa mkataba wa kimaandishi kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Chama Cha Wasafirishaji Dar es Salaam (Darcoboa).Kadhalika, CWT imeiomba serikali kuendeleza utaratibu huo katika mikoa mingine pamoja na kuwapo kwa utaratibu kwa wanafunzi nao wasafiri bure.Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe jana kuhusu utaratibu mpya kwa walimu wa Jiji la Dar es Salaam kusafiri bure kwenye daladala kuanzia Machi 7, mwaka huu.“Tunampongeza sana Mkuu wa Wilaya Paul Makonda, lakini tunaomba kuwapo na mkataba maalum wa makubaliano kwa kuwa tunahofia suala hili lisije likawa la kisiasa zaidi,” alisema Oluoch.Alisema mbali na kuwapo kwa mkataba maalum, piakuwapo kwa makubaliano yatakayowaruhusu walimu wa Jiji la Dar es Salaam kusafiri bure katika mabasi ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (Dart).Alisema kama serikali imedhamiria kuwasaidia walimu, inapaswa kupeleka mkakati huo hata kwa walimu wa mikoani na kuhakikisha walimu hawanyanyapaliwi kama wanafunzi wanavyonyanyaswa.Kuhusu vitambulisho, Oluoch alisema walimu wanapaswa kupewa bure bila ya gharama yoyote na kueleza kuwa visainiwe mkuu wa wilaya.“Kama wanafunzi wananyanyapaliwa vituoni wakiwa na sare za shule, itakuwaje kwa walimu ambao hawavai sare, hivyo tunaomba suala hili liangaliwe vizuri lisije likaleta mkanganyiko,” alisema.Aliongeza kuwa kama Mkoa wa Dar es Salaam umeweza kuwasaidia walimu 19,000 waliopo katika mkoa huo, serikali haiwezi kushindwa kupelea utaratibu huo katika mikoa mingine yenye walimu wachache, akitolea mfano Mkoa wa Mbeya wenye walimu 3,700 na Mkoa wa Mwanza wenye walimu 5,500.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Konondoni, Makonda atakumbukwa na walimU wa Jiji la Dar es Salaam kwa mkakati huo mzuri aliouanzisha kwa walimu na kusema pindi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki akistaafu nafasi yake ichukuliwe na Makonda.Juzi, Makonda alikutana na Darcoboa na kuafikiana kuwa kuanzia Machi 7, mwaka huu, walimu wa shuleza msingi na sekondari wa Jiji la Dar es Salaam, wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia saa11:30 alfajiri hadi saa 2:00 asubuhi na saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni