Walimu Dar kusafiri bure. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatatu, 29 Februari 2016

Walimu Dar kusafiri bure.

Katika kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kutekeleza mpango wa elimu bure, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar es Salaam,  wameamua walimu wa shule za msingi na sekondari kuanzia Machi 7, mwaka huu, kutolipa nauli katika daladala.Mpango huo utaanza kutumika baada ya kukamilika utengenezaji wa vitambulisho maalumu kwa waalimu hao wanaokadiriwa kuwa 10,000.“Ninawatangazia wananchi kuwa kuanzia Machi 7, mwaka huu, walimu wa sekondari na msingi watasafiri bure katika vyombo vya usafiri katika jiji letu la Dar es Salaam,” alisema Makonda.Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabruki, alisema makubaliano hayo ni kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli katika kutekeleza mpango wa elimu bure na kupunguza makali ya maisha kwa walimu hao.Alisema walimu wataanza kusafiri bure kuanzia saa 11:30 alfajiri hadi saa mbili asubuhi, na  saa 9 alasiri hadi saa 11 jioni. Nje ya muda huo, alisema watalazimika kujilipia.“Tujifunze tunapomuona kiongozi kijana anapopenda maendelea inatubidi tumuunge mkono. Makonda tangu aingie Kinondoni ameonyesha nia yadhati ya kuleta maendeleo,” alisema Mabruki.Alisema walimu wote watasafirishwa kwa utaratibu wa vitambulisho na kuwapo na utaratibu wa kila garikuingia walimu wachache.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa