Rais John Magufuli, kwa mara ya kwanza atakutana na wakuu wenzake wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mkutano wa 17 wa kawaida wa jumuiya hiyo, utakaofanyika jijini Arusha keshokutwa.Rais Magufuli ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, jana aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya kwenda Arusha kuhudhuria mkutano huo na kupata mapokezi makubwa, huku akiwashukuru wananchi, watendaji na viongozi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea.Aidha, Rais Magufuli aliwaomba viongozi hao na wananchi kuendelea kujitokeza kuwapokea wageni wengine wakiwamo marais wa nchi zote za Jumuiyaya Afrika Mashariki wanaotarajiwa kuanza kuwasili leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo.Marais wengine wa nchi wanachama wa EAC wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni, Yoweri Museveni wa Uganda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya.
RAIS NKURUNZINZA
Rais Nkurunziza atawasili nchini baada ya miezi 10 ya jaribio la kumpindua Mei mwaka jana.Jaribio hilo lilitokea wakati Rais huyo wa Burundi akiwa jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, mwakajana wakati akiwa bado madarakani.Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuzungumzia mvutano uliokuwapo kati ya Rais Nkurunziza na vyama vya upinzani nchini Burundi vilivyokuwa vikipinga asigombee urais kwa muhula wa tatu.Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Sekretarieti yaAfrika Mashariki, Othieno Owora, jana alithibitisha kuwa Rais Nkurunziza atakuwa miongoni mwama marais wa EAC watakaohudhuria mkutano huo.“Wakuu wote wa nchi wanachama wa EAC wamethibitisha kuhudhuria mkutano huu,” alisema.Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, alithibitishakuwa Rais Nkurunziza atahudhuria mkutano huo.
RAIS MUSEVEN
1Rais Museveni atahudhuria mkutano huo wa viongozi wa EAC ikiwa ni mara ya kwanza na siku chache tangu alipochaguliwa kuongoza Uganda kwamuhula wa tano katika uchaguzi mkuu ulofanyika Februari 18, mwaka huu, ambao unalalamikiwa kuwahaikuwa huru na haki.Akiwa kiwanjani hapo, Rais Magufuli, pia alitoa salama za pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kwa kukamilisha uchaguzi wa viongozi wa kuziba nafasi ya mwenyekiti wa mkoa, katibu mwenezi na mwenyekiti wa vijana, zilizokuwa zimeachwa wazi na waliohamia Chadema, ambao katika uchaguzi huo, Lekule Michael Laizer amechaguliwa kuwa mwenyekiti, Shabani Mdoe (Katibu Mwenezi) na Lengai Olle Sabaya akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa vijana.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Agustine Mahiga, alisema maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yamekamilika na kwamba kikao cha Baraza la Mawaziri kinatarajiwa kuanza leo jijini Arusha .Alisema akiwa Arusha, Rais Magufuli ataongoza viongozi wenzake katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Holili kupitia Taveta na kwa siku mbili za mwanzo atakuwa anaendelea na kazi zake nyingine ambazo hakuzitaja.Ziara ya Magufuli mkoani Arusha ni ya pili tangu achaguliwe kuwa Rais na anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Machi 3, mwaka huu, ingawa Balozi Mahiga, alisema yanaweza pia yakawapo mabadiliko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni