Baada ya serikali kubanwa na wabunge upinzani na kukubali kuondoa mezani hoja ya Mwelekeo wa Mpango wa Pili wa Maendeleo kwa miaka mitano ijayo, Bunge limesema leo utawasilishwa mpango wamwaka mmoja jambo huenda likavuruga tena chombo hicho cha kutunga sheria.Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, aliwaambiawaandishi wa habari jana kwenye viwanja vya Bungekuwa serikali itawasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa mwaka mmoja na si mitano.Alisema baada ya kuwasilishwa, Bunge litakaa kamakamati na kuujadili kwa siku tano kisha mapendekezo yao yatachukuliwa na serikali kwa ajiliya kutengeza mpango wa mwaka mmoja.Alisema mpango huo wa mwaka mmoja utasomwa kwa wabunge Machi 10 na kuwasilishwa tena kwenye chombo hicho cha kutunga sheria wakati wa Bunge la Bajeti.Alipoulizwa juu ya mpango wa miaka, alisema Katiba inasema Bunge linaweza jadili mpango wowote wa muda mfupi au mrefu, kwa hiyo hata kusomwa mpango wa mwaka mmoja ni sawa.Alisema mpango huo wa miaka mitano utafika kwenye chombo hicho cha kutunga sheria siku serikali itakapojisikia.Hali hiyo inatarajiwa kuleta mvutano bungeni kwa sababu wakati Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, na Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe, walivyokuwa wakipinga kuwasilishwa kwa mpango huo Ijumaa iliyopita, walisema inabidi kwanza uje mpango wa miaka mitano ili ndani yake utoke wa mwaka mmoja.Zitto alisema: “Shughuli ya kwanza ya Bunge na RaisMagufuli ni mpango wa maendeleo ya miaka mitano na wameshindwa kwa sababu wameona Bunge halina nguvu sasa wameanza kulipeleka wanavyotaka.“Wameshindwa kujua kwamba limesheheni Wabunge wenye uzoefu, kwa makosa tuliyofanya mwanzo utekelezaji wa mpango unaomaliza muda wake haujafikia asilimia 40, hata wizara ya Magufuli (Ujenzi) ilitekeleza kwa asilimia 53 tu.”Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, Lissu alisema serikali ilianza kuvunja kanuni kwa kutotoa mpango huo siku saba kabla ya mjadala kama ambavyo kanuni zinataka.Kwa upande wake, Lissu alisema kazi ya kwanza ya serikali baada ya kutoka kwenye uchaguzi ni kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa kila mwaka na wa miaka mitano.Alisema jambo hilo liko kikanuni na linalindwa na Ibara ya 63 (3) ya Katiba, hivyo kazi ya Bunge ni kujadili mpango huo na kuuidhinisha.“Sasa wanataka kufunika kombe kama alivyokuwa anataka mwenyekiti (Andrew Chenge). Miaka mitanoiliyopita kwa sababu ya udhaifu wa serikali hatukutunga sheria ya kutekeleza mpango uliopita.“Ukosefu wa weledi wa serikali iliyopita umehamia kwenye hii ya hapa kazi tu (ya awamu ya tano). Bunge kwa mujibu wa orodha ya shughuli wanasema Bunge lijadili mpango na si mwelekeo wala mpango wa muda mfupi,” alisema Lissu.Alisema yote hayo ni matokeo kamati kuvurugwa na kwamba hilo lisingetokea kama wabunge wa kamatiza bajeti waliopita wangekuwemo katika kamati mpya.“Tusiingie kwenye hii aibu kwa sababu kwa sasa hakuna mpango, hakuna sheria, siku tano hizi tutajadili kitu gani? Tutatunga sheria ya kitu gani? Hapa ni kuvuruga ili serikali ya hapa kazi tu isihojiwe,” alisema Lissu.Awali, baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kuwasilisha mapendekezo hayo Ijumaa iliyopita, Zitto aliomba mwongozo wa Spika akisema waziri huyo ametoa hotuba ya Mapendekezo ya Mwelekeo wa Maendeleo wa miakamitano 2016/17 mpaka 2020/21 na alichofanya ni kinyume cha kanuni na bila kugusia ule wa mwaka mmoja.“Maelezo ambayo umeyatoa ili kutuongoza kwenye kuchangia ambayo umeyatoa kanuni ya 94 (1) (4) ni maelezo ya mwaka mmoja, hayahusiani na mpango wa miaka mitano. Tunajadili mpango huu kwa masharti ya Katiba, Ibara ya 63 (3) (C),” alisema na kuinukuu ibara hiyo.Alisema Chenge alitoa maelekezo ya kuchangia hotuba hiyo akitumia Kanuni 94 ya Bunge ambayo inazungumzia mpango wa mwaka mmoja mmoja.“Kanuni zinakukataza kuwahisha shughuli za bunge.Hapa hatujadili mpango wa mwaka mmoja, tunachokijadili kwa sasa ni mpango wa miaka mitano ambao itabidi tuutungie sheria, halafu ndiyo tuje kwenye huo utaratibu ambao upo wewe unaueleza,” alisema Chenge.Naye Lissu wakati akiomba mwongozo, alianza kwa kusoma orodha ya shughuli za Bunge kwa siku hiyo ambapo kwenye ukurasa wa 11 ilikuwa ikisema: “Bunge litajadili na kuidhinisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha mitano 2016/17- 2020/21”.Baada ya kusoma eneo hilo alisema: “Mpango wa Pili wa Maendeleo kwa kipindi hicho uko wapi? Haujawasilishwa. Kanuni ya 94 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, inasema “Bunge litakaa kama Kamati ya Mipango ili kukidhi matakwaya kanuni ya 63 (3) (c) ya Katiba.”Aliendelea kusema: “Tutakaa kwa siku tano hapa tutajadili na kuidhinisha mpango na kuitungia sheria.Muswada wa sheria husika uko wapi? Tutaupitisha lini? Mswada haupo, mpango haupo, tunajadili kitu gani?”Pia alisema Chenge amewaeleza wabunge kwamba baada ya mjadala kamati ya bajeti ndiyo itakayopelekewa mpango.“Nilikuwa naangalia shughuli za kamati ya bajeti, aya ya tisa na nyingine, labda nina mataztizo ya macho lakini ukurasa wa 38 ambapo kazi za kamati ya bajeti zimetajwa sijaona mahali ambapo kamati hii ina mamlaka au majukumu ya kupokea na kujadiliwa mpango wa maendeleo wa taifa.“Hili Bunge lako tukufu linahitaji kuongoza sawasawa. Nina wasiwasi kama unaliekeleza Bunge sawasawa,” alisema Lissu.Chenge alimkatisha Lissu na kusema hoja yake na ile ya Zitto zinafanana na tayari maelezo yake alishayatoa.
SERIKALI YATOA HOJA
Baada ya kutotoa maelezo asubuhi, aliporejea kwenye kikao cha jioni, Chenge alisema hawajakiukaKatiba kama ilivyodaiwa ila utaratibu umekiukwa.Alisema kabla ya kuruhusu hoja hiyo ya serikali kuwasilishwa, kwanza wangetakiwa kukaa kama kamati ya mipango badala kuketi kama Bunge.Alisema pia Bunge lingepaswa kutengua kanuni kwa sababu kanuni hizo zinaelekeza wakae Oktoba na Novemba kupitisha mpango huo.“Nilishtuka sana kwenye hoja ya kuvuja Katiba. Baada ya haya niliyosoma ni wazi kuwa hakuna katiba iliyovunjwa kwa sababu wameleta hapa ili kuwashirikisha wananchi kupitia nyie.“Baada ya kutafakari nimeona ni kweli mpango haujaletwa, kwa hiyo naishauri serikali iondoe hoja iliyoileta kwa mujibu wa Ibara ya 58 (5),” alisema.Naye Dk Mpango, alisimama na kuondoa hoja aliyoiwasilisha kwenye meza ya Spika.Baada ya kutoa hoja hiyo, Chenge aliahirisha Bunge mpaka leo. Kwa mujibu wa kanuni, Bunge lilijiwekea utaratibu wa kufanya kazi mpaka Jumamosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni