Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliingia duru la pili juzi huku mabingwa watetezi, klabu ya Yanga wakipoteza mechi yao ya kwanza msimu huu walipochapwa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union.Hata hivyo, wakati ligi hiyo ambayo mwishowe inatoa bingwa atakayeliwakilisha taifa katika michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika inazidi kushika kasi, tayari kuna malalamiko lukuki kuhusiana na uchezeshaji wa baadhi ya marefa.Hadi sasa kwa mfano, tayari klabu za Simba na Mbeya City zimeshawasilisha malalalmiko kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zikiwashitaki baadhi ya marefa kwa madai ya kusababisha timu zao kufanya vibaya baada ya kuwapendelea wapinzani wao.Mbali na Simba na City, kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, alikwenda mbali zaidi alipotahadharisha kuwa Tanzania haitapata mafanikio kisoka ikiwa TFF itaendelea na 'uzembe' wake kutoifanyia kazi changamoto ya uwapo wa baadhi ya marefa 'mizigo' katika ligi za ndani, hususani ligi ya Bara.Kuna malalamiko kutoka timu nyingine kadhaa ambazo hata hivyo, nyingi hazijawa na ujasiri kama wa Simba na Mbeya City wa kupeleka kilio chao kwa maandishi katika ofisi za TFF, badala yake kulalamika hovyo pembezoni.Ni wazi kuwa baadhi ya malalamiko huwa hayana mashiko, yakitoka kwa wadau wa timu zinazofungwaambazo uzoefu unaonyesha kuwa mara nyingi, wadau wake huwa wagumu kukubaliana na matokeoyanayoziathiri timu zao.Hata hivyo, Nipashe tunaamini kuwa baadhi ya malalamiko hayo ni ya kweli. Tunatambua kwamba kuna jitihada kadhaa za TFF katika kuwasihi marefa wazingatie utoaji wa uamuzi wa haki, baadhi huendelea kufanya kinyume chake, wakizipendelea baadhi ya timu kwa maslahi wanayoyajua wenyewe na kuziathiri timu zisizo na ushawishi wa aina yoyotekwao.Marefa wa aina hii, wenye kuchezesha kwa upendeleo dhidi ya baadhi ya timu, wanaishushia hadhi ligi ya Bara kwa vile kupitia wao, mara nyingi matokeo ya mechi huwa hayaendani na kiwango chasoka kinachoonyeshwa uwanjani.Katika ripoti maalum ya 'upangaji matokeo unavyolitafuna soka la Tanzania' tuliyoichapisha Juni 8-12 mwaka jana, tulieleza namna kadhia hiyo ilivyo hatari kwa soka la Tanzania na maendeleo ya taifa kwa ujumla.Kuendelea kuboronga kwa baadhi ya waamuzi, kamaambavyo iliwahi kudhihirika katika ligi hiyo msimu uliopita pale klabu ya Ruvu Shooting iliposhushwa daraja kwa nguvu na makusudi na marefa, kutalifanya taifa lipate bingwa asiyestahili.Na baada ya kupata bingwa asiyestahili, taifa litapata wawakilishi wasiostahili, na ambao hawatakuwa na jipya kwenye mashindano ya kimataifa na tutaendelea na desturi yetu ya kuwa wasindikizaji.Kwa kutambua athari za kadhia hiyo, tunaishauri TFF ichukue hatua za haraka katika kushughulikia malalamiko yanayozidi kuongezeka kila kukicha, kwani kufumbia macho baadhi ya marefa 'mizigo' katika ligi ya Bara na mashindano mengine ya soka nchini, kutasababisha taifa lianguke zaidi kwenye michuano ya kimataifa.Ni rai yetu pia kwa marefa wa soka nchini kuhakikisha wanachezesha kwa kuzingatia Sheria 17za Soka ili hatimaye taifa lipate wawakilishi sahihi katika mashindano ya kimataifa.Tunatarajia kuona TFF 'inawatumbua' marefa 'mizigo' na wasiokuwa waaminifu kwa manufaa ya mchezo wa soka, ligi ya Bara na maendeleo ya taifa.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni