Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fedrick Shoo ‘amemkomalia’ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimweleza viongozi wa dini na Watanzania wanavyosikitishwa na kuumizwa na kitendo cha askari wa majeshi kuingizwa ndani ya ukumbi wa Bunge.Askofu Dk. Shoo alisema hayo jana katika hotuba yake aliyoitoa mjini hapa katika ibada maalumu ya kuingizwa kazini iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Moshi mjini.Bila ya kumung’unya maneno, alisema Watanzania hawajafurahishwa kuona Bunge, ambayo ni nyumba ya demokrasia ikichezewa.Alisema ingawa wanaamini hoja hujadiliwa na kuamuliwa kwa njia ya demokrasia, hali iliyojitokeza siku chache zilizopita inasikitisha.Chanzo cha tukio hilo ambalo askari zaidi ya 50 waliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kuwatoa kwa kuwabeba wabunge wa upinzani ni kutokana na kukataa amri ya Mwenyekiti wa Bunge la 11, Andrew Chenge ya kuwataka watoke kwa hiari, ni kauli iliyotolewa na serikali kwamba Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.Akionyesha dhahiri maaskofu 24 wanaounda dayosisi za kanisa hilo, wachungaji na Watanzania walivyofedheheshwa na hali hiyo alisema: “Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunasikitika sana na hali inayoendelea katika Bunge letu. Bunge ni nyumba ya demokrasia, kwa hiyo Watanzania tunatarajia kuona na kusikia hoja zinajadiliwa kwa uwazi na katika hali ya kistaarabu," alisema na kuongeza:"Heshima hii ya Bunge kama nyumba ya demokrasia haiingizwi majeshi, kwa hiyo tunaomba wabunge naowatunze heshima yao na Bunge liheshimiwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ndiwe kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni. Tunaamini kwamba hilolitatunzika na sisi (maaskofu) tutakuombea kwa Mungu.”Majaliwa alihudhuria ya kuingizwa kazini kwa Askofu Dk. Shoo akimwakilisha Rais Dk. John Magufuli. Askofu Dk. Shoo ambaye anachukua nafasi ya Askofu Dk. Alex Malasusa aliyemaliza muda wake, ataiongoza KKKT kwa kipindi cha miakaminne ijayo.Hata hivyo, Dk. Malasusa aliyeliongoza kanisa hilo kwa miaka minane mfululizo, ataendelea kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.Aidha, Askofu Dk. Shoo alisema viongozi wa dini wanaiomba serikali ifikirie upya mchakato wa Katibampya na kama yapo majeraha yashughulikiwe na mchakato uendelee ili kuijenga Tanzania ijayo.Pia alitaka suala la Zanzibar lishughulikiwe na kusema alisema mgogoro huo usipodhibitiwa unaweza kulitia taifa doa na kwamba akiwa Mkuu wa KKKT, yuko tayari kutoa ushauri wake iwapo utahitajika.MAJALIWA ALONGAAkijibu hoja zilizotolewa na Mkuu wa Kanisa hilo, Majaliwa alisema serikali imesikia na itaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na mhimili huo wa Bunge.“Mheshimiwa Baba Askofu na Mkuu wa Kanisa, katika hotuba yako ulitaka serikali isiingilie mhimili wa Bunge na ukataka mihimili yote mitatu ambayo niBunge, Mahakama na Serikali viheshimiane. Katika Bunge hili tutahakikisha demokrasia inaheshimiwa.Tutajenga nidhamu, kusimamia lugha nzuri na matendo yetu, hilo nakuhakikishia,” alisema.Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, Waziri Mkuu alimwahidi Askofu Dk. Shoo, maaskofu wengine, wachungaji na waumini wa madhehebu mbalimbali kwamba amelipokea ombi hilo na atalifikisha kwa Rais Dk. John Magufuli.“Kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli, amenituma hapa kumwakilisha kwa nia njema kabisa, nitakwenda vivyo hivyo kumweleza yale yote ambayo mmeyashauri, likiwamo suala la kufufua reli,kupambana na umaskini na kuinua uchumi wa taifa,”alisisitiza Majaliwa.Awali, akiongoza ibada hiyo ya kumwingiza kazini Askofu Dk. Shoo, aliyekuwa Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Malasusa, alisema Dk. Shoo alichaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 19 wa Kanisa uliofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Arusha kati ya Agosti 12 na 14, mwaka jana.Dk. Malasusa alisema kanisa hilo linamwomba Mwenyezi Mungu amjalie Dk. Shoo hekima ili aweze kutoa uamuzi sahihi, wa kweli, haki na unaoleta faraja na amani kwa kanisa, pia ajaliwe kuona mahali penye dhuluma, uonevu, ukandamizaji na mateso ya kila aina ili haki itiririke kama maji.Baada ya kutamka maneno hayo, Askofu Dk. Malasusa alimkabidhi Askofu Dk. Shoo Katiba ambayo ni andiko rasmi lenye mwongozo, utaratibu na utawala wa KKKT.Viongozi mbalimbali, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais wa Chama chaDemokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, walihudhuria.Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Regnald Mengi.Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala na wabunge Godbless Lema (Arusha Mjini-Chadema), Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini-CCM), James Mbatia (Vunjo-NCCR Mageuzi), Anthony Komu (Moshi Vijijini) na Japhary Michael (Moshi Mjini) wote kupitia Chadema.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni