Mbarawa ang'oa vigogo TCRA - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 20 Februari 2016

Mbarawa ang'oa vigogo TCRA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewasimamisha kazi na kuwastaafisha maofisa watatu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa tuhuma za kuhujumu mtambo wa mawasiliano na kuisababishiaserikali hasara ya Sh. bilioni nne.Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Profesa Mbarawa  aliwataja maofisa hao kuwa ni Mkurugenzi wa Sheria wa  TCRA, Elizabeth Nzagi, Mwanasheria  Modester Ndunguru na aliyekuwa msimamizi wa mtambo huo, Mhandisi Richard Sunday.Alisema kuna kifaa cha kubaini gharama za mawasiliano ya kila simu nchini ili kujua kampuni zinapata kiasi gani kilipaswa kufungwa kwa muda mrefu, lakini hakikufugwa kwa sababu zisizojulikana.“Mkataba ulisema kifugwe ili tujue gharama za mawasiliano lakini hakikufugwa na badala yake kujua gharama imetegemea kampuni za simu pekee, huku simu za nje serikali ikijua gharama husika,” alisema.Alisema maofisa hao watakuwa nje ya vituo vyao vya kazi wakati uchunguzi ukiendelea kwa hatua zaidi.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa