Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), jana lilitangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, yakionyesha asilimia kubwa ya wanafunzi kufeli.Matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, yanaonyesha kwamba hali ni mbaya kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi takribani robo tatu kufeli.Kwa mujibu wa matokeo hayo, waliofaulu kwa darajala kwanza mpaka la tatu ambao kimsingi ndiyo waliofaulu ni asilimia 25 huku wale waliopata daraja la sifuri na nne ambao wamefeli ni asilimia 74.66.Waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, watahiniwa 31,986 sawa na asilimia 9.01 walipata daraja la pili, sawa na asilimia 6.69. Waliopata daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56. Waliopata daraja la nne ni 151,067 sawa na asilimia 42.57 na waliopata daraja sifuri ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.Uhalisia wa matokeo hayo ni kuwa ni mabaya na ni aibu kwa Taifa. Hilo linadhihirishwa na kauli ya Dk. Msonde kwa gazeti hili baada ya kutangaza matokeohayo kwamba hali ni mbaya kwani ingetakiwa walau wale waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu wafikie asilimia 50.Hali ingekuwa hivyo kungekuwapo na unafuu kwa kuwa wanaofaulu kwa ngazi ya daraja la kwanza hadi la tatu ndio wanaopata fursa ya kujiunga na kidato cha tano na nafasi zingine za vyuo.Siyo vizuri kulinganisha matokeo ya mwaka 2015 na ya mwaka 2014 ambayo ufaulu wake umeshuka kwaasilimia 1.85, lakini suala la msingi ni kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wamefeli.Mbali na matokeo ya jumla kuwa mabaya, lakini pia ufaulu mbaya wa somo la Hisabati umeendelea kubainika miongoni mwa wanafunzi wengi. Ni asilimia 16.76 aliofaulu somo hilo huku asilimia 83.24 wakifeli. Katika masomo ya Biashara pia ufaulu umekuwa chini ya asilimia 50.Kuendelea kushuka kwa ufaulu wa somo la Hisabati kunaonyesha jinsi gani taifa linavyokabiliwa na changamoto kubwa kutokana na umuhimu wa somo hilo ambalo ni msingi wa kila mwanafunzi ambaye ana matarajio ya kuendelea na masomo ya juu.Tunasema kuwa somo hilo ni msingi kwa kila mwanafunzi kwa sababu wale wenye ndoto za kusoma Sayansi au Biashara ni lazima walisome na kufaulu katika masomo ya kidato cha tano na sita nabaadaye ngazi ya elimu ya juu.Matokeo haya yanapaswa kuchukuliwa na kila mmoja kama changamoto kubwa na ngumu inayolikabili taifa kwa sasa. Hakuna hatua za kuchukua kubadili hali hiyo zaidi ya kuboresha mazingira ya ufundishaji.Moja ya sababu za matokeo hayo mabaya zilizoelezwa na wadau kadhaa wa elimu ni kwamba walimu hawajawezesha kuwa na viwango bora vya kutoa elimu kwa watoto wetu. Haiwezekani tukapata matokeo mazuri kama walimu hawana uwezo wa kufundisha pamoja na kutokuwa na morali.Huko nyuma baadhi ya jitihada zilifanywa na serikali ya awamu ya nne kwa kuiweka iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika wizara zuilizoanza katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Miongoni mwa malengo yaliyokuwa yamepangiwa wizara hiyo ni kuongeza viwango vya ufaulu.Kupitia utaratibu wa kubadili mfumo wa kutoa matokeo kutoka madaraja kwenda GPA, ufaulu ulikuwa unaonekana kupanda kila mwaka, ingawa wadau wa elimu hawakuridhishwa na mfumo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa unawabebe wanafunzi katika matokeo kuliko uhalisia wa uwezo wao.Uamuzi wa kurejeshwa mfumo wa madaraja tunaamini kuwa ni mzuri na uendelee kutumika, isipokuwa serikali iendelee kuwekeza katika shule kwa kuwajengea walimu mazingira mazuri ili wawe na uwezo na morali wa kufundisha watoto wetu na wapate matokeo mazuri.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni