Takukuru yabaini unadhirifu bn1/- Kinondoni - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 31 Januari 2016

Takukuru yabaini unadhirifu bn1/- Kinondoni

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika Manispaa ya Kinondoni umegundua ubadhirifu wa Sh. Milioni 924.8 wakati wa urasilimishaji ardhi, katika kata nne uliofanywa na watendaji wa serikali wilayani humo.Ubadhirifu huo uliibuliwa juzi jijini Dar es Salaam katika kikao cha wadau, wakiwemo watendaji na madiwani, kilicholenga kujadili utafiti huo uliofanywana Takukuru kwa miezi nane kuanzia mwezi Mei mwaka jana.Akiwasilisha utafiti huyo mbele ya wadau, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa huo, Denis Manumbu alisema kata ambazo watendaji wake wamekumbwana kashfa ni Kwembe, Kimara, Kibamba na Saranga ambao sasa wanachunguzwa.Manumbu ambaye pia ni mtafiti, alisema urasilimishaji wa ardhi Manispaa ya Kinondoni ulifanyika katika kata hizo ambapo kila moja ilifungua akaunti maalum ya kuweka fedha hizo na kwamba akaunti hizo zilikuwa zikisimamiwa na Ofisa Mtendaji wa kata husika.“Baada ya Manispaa kufanya ukaguzi wa hesabu za urasilimishaji zilizoainisha hoja za ukaguzi na mapendekezo ya kudhibiti upotevu wa fedha hizi, vitendo vya rushwa bado viliendelea kwenye Manispaa hii,” alisema.Alisema kuwa vitendo vya rushwa vilivyofanywa na watu hao ni matumizi mabaya ya mamlaka, kujipatiamanufaa, wizi, udanganyifu wa nyaraka na kula njama kuwezesha kosa la rushwa kufanyika.Manumbu alisema vitendo hivyo ndivyo vilivyosababisha Takukuru kufanya utafiti ambao umethibitisha kuwepo kwa rushwa katika mchakato wa upokeaji na utumiaji wa fedha zilizochangwa na wannachi kwa ajili ya kurasilimishiwa maeneo ya ardhi zao.Imebainika kuwa watendaji wa serikali walitumia vibaya madaraka yao na kujipatia manufaa ya fedha za serikali ambazo wamezitumia kwa maslahi yao binafsi, alisema Manumbu, na kwamba wamebaini watendaji kufanya udanganyifu kwenye nyaraka, wizina ubadhilifu wa fedha za serikali.“Vitendo hivi vimetokea kutokana na udhaifu wa kusimamia sheria ya fedha za serikali za mitaa, udhaifu wa usimamizi wa operesheni ya urasilimishaji,” alisema na kuongeza:“Ubadhilifu huu ulifanywa na Ofisi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, Ofisi ya Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni na ofisi ya maafisa watendaji wa kata eneo la urasilimishaji,” alisema.Alibainisha kuwa vitendo hivyo vimesababisha ufanisi wa urasilimishaji mijini katika Manispaa hiyo kuwa duni kutokana na baadhi ya wananchi kuchangia fedha ili wapimiwe maeneo yao na kuliwa huku meneo yao yakibaki bila kupimwa.Pia alisema wamebaini maeneo ambayo yalibahatika kupimwa, wananchi hawakupewa hati miliki ya ardhi na yale ya huduma za kijamii mengi yakiwa na miradi hewa.Alisema  watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya mitaa, kata na idara ya mipango miji na ofisi ya Mkurugenzi Manispaa hiyo wamekuwa wakitumia mamlaka zao vibaya ili kujipatia manufaa ya fedha ama wao wenyewe au watu wengine.Aidha, alisema watu hao wamekuwa wakifanya ubadhirifu wa fedha za urasilimishaji wa ardhi na kusababisha miradi kusuasua wakati michango ya wananchi ya urasimishaji hupokewa ofisi ya kata na kuhujumiwa kwa kutowekwa katika akaunti husika.Alisema katika kata ya Kwembe Sh. Milioni 13.3 zilipokelewa  na ofisi ya ofisa Mtendaji wake kati ya mwaka 2012 hadi 2014 kutoka kwa wananchi kwa ajili ya kurasilimishiwa maeneo yao.Alisema kiasi hicho cha fedha hakipo kwenye akauntiwala ofisi ya mtendaji huyo na kwamba maeneo ya ardhi ya wananchi hayajapimwa.Pia utafiti huo umebaini, ofisi ya mtendaji huyo imetengeneza vitabu vya kukusanya fedha bila idhini ya Manispaa husika na kwamba risiti zake zilikuwa zikitolewa za vitabu viwili tofauti.“Urasilimishaji unasimamiwa na watendaji wa kata, mkuu wa idara ya mipango miji na maofisa wake walikuwa wanafanya kazi za kiutaalam, masuala yote yanayohusu fedha wahusika ni Ofisa Mtendaji Kata," alifafanua.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa