Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 24 Januari 2016

Nape Nnauye: Kasi Ya Rais Magufuli Itaviua Vyama Vya Upinzani Hapa Nchini

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendeleakuwepo.Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu huyo wakati alipokuwa akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 39 ya CCM ambayo kilele chake kimepangwa kufanyika mkoani hapa Februari 6, mwaka huu badala ya Februari 5 iliyozoeleka.Alisema kuwa chama kimelazimika kubadili tarehe ya kilele ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo maadhimishohayo kwa kufanya kazi badala ya kuwa na sherehe mbalimbali.“Maadhimisho ya safari hii ni tofauti na ya miaka mingine. Safari hii wananchi watatakiwa kushiriki zaidi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo. Kauli mbiu yetu ni ‘Sasa kazi’ hivyo watu wafanye kazi ili wajiletee maendeleo yao wenyewe,”alisema.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa