Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Januari, 2016 ametunuku kamisheni kwa Maafisa wapya 205 wa jeshi la wananchi kundi la 57/15 katika Chuo cha mafunzo ya kijeshi (TMA) Monduli Mkoani Arusha.Maafisa hao wapya wametunukiwa cheo cha Luteni Usu, ambapo kati yao 16 ni maafisa wanawake, na 189 ni maafisa wanaume.Aidha, miongoni mwa maafisa wapya 205 waliotunukiwa kamisheni, maafisa 10 wametoka majeshi rafiki kutoka nchi za Uganda, Kenya na Burundi.Akiwa katika uwanja wa paredi wa chuo hicho Rais Magufuli amepokea heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa wimbo wa Taifa na kukagua gwaride rasmi lililojumuisha maafisa hao wapya.Baada ya kutunukiwa kamisheni, Maafisa wapya wa jeshi wamekula kiapo na wametoa heshima kwa gwaride lililopita mbele ya Rais kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka.Viongozi wengine waliokuwepo katika tukio hilo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Maafisa wangazi za juu jeshini na Maafisa wastaafu, viongozi wa mkoa na wilaya na wakufunzi kutoka nje ya nchi.Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoa kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la wananchi tangu achaguliwe kuwaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Oktoba Mwaka jana.Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULUArusha.23 Januari, 2016.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jumapili, 24 Januari 2016

Home
Unlabelled
Amiri Jeshi Mkuu Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli Atunuku Kamisheni Kwa MaafisaWapya 205 Wa Jeshi La Wananchi
Amiri Jeshi Mkuu Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli Atunuku Kamisheni Kwa MaafisaWapya 205 Wa Jeshi La Wananchi
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni