Mshauri ada elekezi apatikana - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 31 Januari 2016

Mshauri ada elekezi apatikana

Serikali imepata mshauri kutoka Chuo Kikuu Huria cha jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa mfumo wa ada elekezi na nini kifanyike.Aidha, serikali imesema inaandaa mpango mpya wa ada elekezi ambao utakuwa na mafungu tofauti; kulingana na ubora wa shule husika.Akizungumza jana Bungeni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alisema mshauri huyo ametakiwa kuwasilisha ripoti hiyo ifikapo Machi.Alisema baada ya uchambuzi huo, wamiliki wa shulewataitwa wizarani kwa ajili ya kuwasilisha michangoyao, ikiwemo uthibitisho wa ada wanazozitoza.Profesa Ndalichako alisema serikali inatambua kuna ulanguzi wa ada, lakini pia kuna shule zinatumia gharama kubwa kujiendesha.Alisema baadhi ya shule zinawalipa walimu wake mpaka Sh. milioni 2 kwa mwezi wakati nyingine ni Sh. 500,000.“Huduma zinazotolewa shuleni unakuta zipo tofauti,"alisema Profesa Ndalichako. "Kuna shule nyinyine zina hadi swimming pool, zimejengwa kwa terazo, unapokuwa unatoa ada elekezi ni lazima uzingatie kwamba mwanafunzi anasoma katika aina gani ya shule.“Kuna shule nyingine binafsi ambazo hazina hata sakafu hivyo huwezi kuja na ada elekezi ambayo utasema ni shilingi kadhaa. Ni lazima tuangalie,  hata chakula wanachopatiwa wanafunzi kinatofautiana."Kuna shule nyingine wanafunzi wanapewa hadi soseji, wanakula pilau kila siku na wengine wanakulaugali na maharage kila siku. Hivyo huwezi ukaja na ada elekezi ambayo ni ya pamoja.”

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa