Je furaha inaweza kuwa na sauti gani ?
Ni swali linaloulizwa na Umoja wa Mataifa ukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya furaha duniani, tarehe 20 Machi.Kwa maana hiyo Umoja wa Mataifa umezindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayoitwa ''#HappySoundsLike''
yaani “Sauti ya Furaha” ukiiomba jamii ya kimataifa kuchagua wimbo bora unaomfanya mtu kufurahi zaidi.
“Kwenye siku hii, tunatumia lugha ya kimataifa ya muziki kuonyesha mshikamano na mabilioni ya watu duniani wanaoathirika na umaskini,
ukiukwaji wa haki za binadamu, mizozo ya kibinadamu na matokeo ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi”
Aidha amesema kwa upande wake wimbo anoupenda zaidi ni “Signed Sealed Delivered” wa Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, Stevie Wonder.
Miongoni mwa wasaani watakaoshiriki kwenye maadhimisho hayo mwishoni mwa wiki hii mabalozi wa umoja wa mataifa
Charlize Theron, Lang Lang, Michael Douglas, Midori, Jean-Michel Jarre na Angelique Kidjo pamoja na wasaani maarufu kama David Guetta, Cody Simpson na Pharrell Williams.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni