Clouds Media Group imeamua kutengeneza daraja kubwa lililokuwa linakosekana kuwaunganisha wafanyakazi wake na wasikilizaji wao kwa kutoa copy za bure za jarida linaloitwa "Mjengoni" litakalokuwa likitoka kila mwezi
Newsletter hiyo itakuwa ikikupa kuwaelewa zaidi watangazaji, producers
na wafanyakazi wengine kiundani zaidi na si kwa kuwasikia tu.Mjengoni
toleo la kwanza tayari limeshatoka, na mtangazaji wa Power Breakfast
"Gerald Hando" ndie
aliebeba cover ya jarida hilo, huku ndani kukiwa na story pamoja na interview ya mtangazaji wa Clouds TV "Shadee" na producer wa long time kitambo Boniventure Kilosa a.k.a Dj Venture.
Mjengoni linapatikana ndani ya jarida jipya la Kitangoma, Mlimani City,
Quality Plaza n akatika mabasi yanayoenda mikoa ya Kilimanjaro, Arusha,
Mbeya, Mwanza, Morogoro na Kampal.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni