Msanii msomi na msemaji mkuu kutoka kundi la Weusi Nikki wa pili,
amewajia juu kundi la vijana wanaosadikiwa kufanya fujo katika mdahalo
wa pili ulioandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere ili kuielewa kwa
kina katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na bunge maalum la
katiba.
Kongamano hilo lililofanyika jana ndani ya ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo
Plaza liliingia dosari na vurugu kubwa mpaka kupelekea polisi kuingilia
kati na kutuliza fujo hizo kwa mabomu ya machozi, baada ya kundi la
vijana kusadikiwa kuanzisha fujo huku wakiwa na mabango mbali mbali,
wakiimba CCM,CCM,CCM na "Kama sio juhudi zako Nyerere Warioba angekuwa
wapi na kuhamia jukwaani kuendeleza fujo hata kupelekea kusitishwa kwa
kongamano hilo
Kutokana na hali hiyo kutokea, Nikki ameandika ujumbe
huu kwa vijana kupitia acc yake ya Instagram akilaani kitendo
alichofanyiwa Warioba

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni