Msichan mmoja anayeitwa Aisha ambaye imesemekana amekuwa akieneza maneno ya
uongo kuhusiana na watu mbalimbali, amejikuta katika wakati mgumu baada
ya kusutwa na wanawake kutokana na vitendo hivyo.
Siku aliyobainika wanawake hao wamesema
Aisha alimpigia simu mwenzake mmoja kwamba kuna kundi la wanawake wapo
saluni wanamsema na baada ya kufika wakabaini kuwa msichana huyo ndiye
aliyesema.
Wanawake waliokuwa katika tukio hilo
wamesema kutokana na tabia hiyo alishindwa kuishi na mama yake na
kupokelewa na mama yake wa hiari ambaye naye amesema kuwa kutokana na
tabia za msichana huyo amelazimika kumfukuza.
Wakati wanawake hao wakisema namna
ambavyo amekuwa akieneza uongo huo, Aisha hakuwa na neno lolote
kujitetea kama ni kweli au hapana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni