NIPASHE
Mwanamke mmoja Swaumu Aboubakari mwenye miaka24 mkazi wa Keko Jijini Dar es salaam ambaye ni mjamzito amenusurika kufa baada kupigwa na vitu vyenye ncha kali na mzazi mwenzake kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Akizungumza kwa shida katika wodi alikolazwa Hospitali ya Mwananyamala alisema ameishi na mzazi mwenzake kwa takribani miaka mitano huku ndoa yao ikitawaliwa na migogoro kila wakati.
Alisema baada ya Mateso kuongezeka alichukua uamuzi wa kurudi nyumbani kwa wazazi wake akiwa na mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja huku akiwa na ujauzito mwingine.
Alisema juzi usiku alitoka Keko kwenda Tandale kwa mzazi mwenzake kwa ajili ya kuomba fedha za matumizi lakini akiwa ndani ya nyumba yake mwanaume huyo alitoka sebuleni na kumchukua kwa nguvu mtoto na kwenda kumlaza chumbani na aliporudi alianzisha ugomvi akishirikiana na ndugu zake akimuhumu mwanamke huyo kuwa mimba si yake.
“Mume wangu bila hata huruma akishirikiana na ndugu zake walinipiga kwa kutumia waya,rungu,fimbo na chuma,sehemu mbalimbali za mwili na nimejaa vidonga kama mnavyoona”alisema Mwanamke huyo.
NIPASHE
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wanaojiuza miili yao Zanzibar maarufu kama madada poa yameongezeka kutoka asilimia 10 hadi19 hali ambayo inaonyesha kuwa Ukimwi bado ni tishio.
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Abdulhabib Fereji alisema kiwango cha maambukizi ya Ukimwi Zanzibar kimefikia asilimia moja kutoka asimilia 0.6.
Alisema maambukizi yapo juu zaidi hasa katika makundi maalum likiwemo la wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kuwa maambukizi hayo kwa mwaka 2007 yalikua asilimia12 hadi kufikia asilimia 2.6 mwaka 2012.
Alisema kwa vijana wanaotumia dawa za kulevya,maambukizi yalikua asilimia 16 hadi asilimia 11.3 na alisema yanaongezeka kutokana na Zanzibar imezungukwa na mazingira hatarishi na kuwa mabadiliko ya haraka ya tabia za kufanya maamuzi sahihi ndani ya jamii katika kukabiliana na maambukizi mapya.
MWANANCHI
Baadhi ya maeneo nchini yalikosa umeme kwa siku nzima ya jana,kitendo kilichotafsiriwa na wengi kwamba ni hujuma ili kuwafanya wasione mmjadala wa kashfa ya IPTL uliokua ukiendelea bungeni Dodoma jana.
Taarifa zilieleza kwamba maeneo mengi katika miji ya Mbeya,Arusha,Mwanza,Manyara,Tanga,Singida,Tabora,Morogoro,Shinyanga na Pwani na baadhi ya Mikoa mingine haikua na huduma hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Felchesmi Mramba alithibitisha kukatika kwa umeme katika maeneo mengi hapa nchini lakini alikanusha kuwa siyo hujuma kuwafanya wananchi wasipate matangazo ya moja kwa moja toka bungeni.
Alisema kukatika kwa umeme kunatokana na matatizo ya moja ya mitambo kati ya mitambo mitatu ya kuzalisha umeme kwenye bwawa la kidatu Morogoro.
MWANANCHI
Wizara ya Maliasili na Utalii imepiga marufuku uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Waziri wa Wizara hiyo Lazaro Nyalandu alitoa tamko hilo juzi wakati akizindua vivutio vipya vya utalii vilivyopo ndani ya ziwa Manyarana ni njia ya kupitia watalii juu ya chemchem ya maji moto na njia ya kuoa viboko wanaoishi ndani ya ziwa hilo.
Njia hiyo ya juu ambayo iligharimu kiasi cha milioni175 ina urefu wa mita 650 na inawezesha kuona viumbe hai na ndege aina ya ya flamingo kwa urais kabisa.
Nyalandu alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yoyote kuingia na kuchimba madini ya hifadhi hiyo inayodaiwa kuwa ipo hatarini kutoweka kutokana na shughuli nyingi za kibinadamu kuingilia.
MWANANCHI
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeingia katika mgogoro na wafanyakazi wake ambao wanadai zaidi ya milioni125 za malimbikizo ya likizo,katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Katika madai hayo ambayo yapo kwenye taarifa waliyoikabidhi kwa uongozi wa hospitali hiyo,wafanyakazi hao wameutaka ueleze sababu za wao kutolipwa kwa wakati kinyume na makubaliano ya mikataba ya ajira zao inayoelekeza kuwa walipwe kabla ya kuanza likizo.
“Tunautaka uongozi utupe majibu ya haraka kwa nini umeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake nauli za likizo zao,hali hii inawaumiza sana wafanyakazi wengi bila sababu za msingi,”ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Wafanyakazi hao wanalalamikia pia kutopewa stahiki zao zinazotokana na malipo yanayotokana na faida inayotokana na mfuko wa Bima ya afya,ambayo hutakiwa kulipwa kwa asilimia40 ya malipo hayo kutoka na huduma wanazotoa.
MWANANCHI
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jana iliwaachia huru washtakiwa wa kesi ya EPA baada ya kuwaona kwamba hawana hatia katika mashtaka ya manne yaliyokua yakiwakabili,likiwemo la wizi wa shilingi 2.2 bilioni za akaunti ya madeni ya nje iliyopo benki kuu.
Baada ya kuachiwa huru,washtakiwa hao ambao muda wote wakati wa hukumu walikuwa wanaonekana kusali waliondoka mbio mahakamani hapo huku wakiwa hawaamini kilichotokea.
Lema ambaye alikua Mkurugenzi mtendaji wa Njake Hotel na mwenzake Munis walikuawakikabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kuiba BoT,kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu na kutoa nyaraka za uongo.
Hata hivyo walikana kuifahamu kampuni kutoka Japan ambayo inadaiwa kuwa ilirithisha kampuni yake kiasi hicho cha fedha bilioni 2.2 za EPA
MWANANCHI
Wakati shughuli ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kurawa Serikali za mitaa ikiendelea nchini,hali si shwari kutokana na wananchi wengi kutoelewa kinachoendelea huku idadi ndogo ya wananchi ikijitokeza.
Uchache wa waliojitokeza mkoani Simiyu unaelezwa kusababishwa na kutokuwepo kwa matangazo na hamasa ya kutosha.
Zaidi ya vtuo 10 vilivyotembelewa na katika halmashauri ya mjiwa Bariadi, havikua na watu zaidi ya mawakala wavyama na makarani.
Baadhi ya mawakala wa vyama vya Chadema na CCM wameilalamikia ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kutoa taarifa kwa wananchi badala yake kazi hiyo wameachiwa.
JAMBOLEO
Kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow imedaiwa kuwagawa Wabunge wa CCM katika kikao chao kilichohudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Philip Mangula huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akigoma kuwajibika kwa maelezo kuwa Bunge halina mamlaka ya kumwajibisha zaidi ya aliyemteua.
Mmoja wa wabunge aliyehudhuria kikao hicho alisema Waziri wa Nishati Sospter Muhongo na Jaji Werema walipewa nafasi ya kujitetea kwa kuwa wamekua wakitajwa kweye kashfa hiyo.
Katika utetezi wake Werema alidai kuwataratibu zote za utoaji fedha kwenye akaunti hiyo zilifuatwa na kuwashangaa wabunge kwa kuwa waoga kwa kuwa yeye si mwoga na kamwe hawezi kujiuzulu.
Kwa upande wa Muhongo alitumia fursa hiyo kujikita zaidi katika kusimulia jinsi IPTL ilivyoingia nchi hadi kufikia hatua ya sasa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni